ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 10, 2017

MISHAHARA YA RAIS, MAWAZIRI NA MAGAVANA KENYE YAPUNGUZWA.


Tume ya Mishahara na Marupurupu ya Watumishi wa Umma nchini Kenya imetangaza kupunguzwa kwa mishahara ya maafisa wakuu wa serikali wakiwemo rais, mawaziri na magavana.
Mwenyekiti wa tume hiyo Bi Sarah Serem ametoa mpangilio mpya wa malipo ambao anasema utaokoa jumla ya Sh8 bilioni (dola milioni  80 za Marekani) kila mwaka na kupunguza jumla ya mishahara inayolipwa watumishi wa umma kwa asilimia 35.
Kwa mujibu wa tangazo la Tume ya Mishahara na Marupurupu ya Watumishi wa Umma nchini Kenya sasa Rais wa nchi atakuwa akilipwa Sh1.4 milioni (sawa na dola 14,000) kila mwezi, badala ya Sh1.65 milioni (dola 16,500), huku naibu wake akipokea Sh1.2 milioni (dola 12,000).
Aidha taarifa hiyo ya Tume ya SRC imeeleza kuwa, mawaziri watakuwa wakilipwa Sh924,000 (dola 9,200), Spika wa Bunge Sh1.1 milioni (dola 11,000) nao magavana wa kaunti Sh924,000 (dola 9,240). Mabadiliko hayo yataanza kutekelezwa tarehe 8 Agosti, 2017.
Rais Uhuru Kenyattaf na naibu wake William Ruto.
Tume hiyo imependekeza kufutiliwa mbali kwa marupurupu ya kipimo cha usafiri wa magari kwa magavana na wabunge na badala yake hilo litakuwa likifidiwa na mfumo mpya wa marupurupu kwa kuzingatia kanda. Bi Sarah Serem amesema kuwa, maafisa wa serikali walikuwa wakitumia vibaya mfumo wa marupurupu wa kupimiwa usafiri wa magari.
 
Magavana na manaibu wa magavana pia hawatakuwa wakilipwa tena marupurupu. Wabunge, ambao wamekuwa wakilipwa marupurupu kwa kuhudhuria vikao vya kamati mbalimbali, pia watakosa marupurupu hayo. Viongozi wa serikali ya upinzani bungeni, ambao pia walikuwa wakipokea marupurupu ya majukumu maalum pia hawatalipwa tena marupurupu hayo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.