ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, June 1, 2017

MWILI WA SHABIKI WA SIMBA SHOSE FIDELIS WAAGWA LEO DARNa Abog: JEMBE FM
Mashabiki na viongozi  wa klabu ya Simba leo wameungana na wanafamilia wa aliyekuwa shabiki kindakindaki wa klabu hiyo Shose Fidelis Masao, kuuaga mwili wake kwenye Ibada iliyofanyika majira ya Saba hadi saa Tisa mchana, kwenye kanisa la Roman Catholic Magomeni jijini Dar es salaam.

Shose alifariki kwa ajali ya gari Mei 29, eneo la Dumira mkoani Morogoro alipokuwa akitokea Dodoma kuishabikia klabu hiyo kwenye mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho. Katika gari hilo alikuwa na kiungo na nahodha wa Simba Jonas Mkude ambaye alinusurika pamoja na wengine wawili.

Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva amesema klabu itamuenzi shabiki huyo na watamkumbuka daima kwani msiba wake umewagusa wanasimba wote pamoja na jamii ya wapenda soka wote Tanzania.

Marehemu Shose alizaliwa 1988, Ilala, Dar es salaam na mwili wake utasafirishwa kwenda mkoani Kilimanjaro kwa mazishi. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe. Amen.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.