ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 8, 2016

UANDISHI WA HABARI KWA TAKWIMU, SILAHA YA MWANDISHI BORA WA ZAMA ZA LEO.


Na:  Edwin  Soko
Jahannesburg
Afrika  ya  Kusini

Mkutano  wa  kimataifa  wa  bara  la  Afrika  juu  ya  uandishi  wa habari  za  uchunguzi  umeanza  leo  Mjini  Jahannesburg    Afrika  ya  kusini kwa  Waandishi   wa habari    toka  Nchi  mbalimbali  kushiriki  wakiwemo wanaotoka  Nchini Tanzania.

Mkutano  huo  wa siku tatu  kuanzia  Novemba 7hadi  9, 2016  unafanyika  kwenye  Chuo  Kikuu  cha  Wits  kilichopo  Jahannesburg   huku  malengo makuu  yakiwa  ni  kuwaleta  Waandishi  pamoja  ili washiriki  kwenye  kujadili  matatizo  ya kitaaluma  yanayoikabili  tasnia  ya  habari  Afrika  hasa wakati wa kuripoti  habari  za  uchunguzi.

Akiongea  na  Waandishi wa  habari  wanaoiwakilisha  Tanzania  kwenye  mkutano huo, Mkurugenzi  wa  Wakfu  wa Tasnia ya  Habari  Tanzania, Bw.  Earnest  Sungura  amesema kuwa, mkutano  huo   untawapa  fursa   washiriki  toka  Tanzania  kujifunza  changamoto za  uandishi wa  kiuchunguzi toka  kwa  washiriki  wa Nchi  mbalimbali  na kubadilishana  uzoefu.

“Lengo  la    kuwachagua  miongoni  mwenu  ili  mhudhurie mkutano  huu  ni  kutaka  kuongeza  thamani  za kazi  zenu  mnazozifanya  kwenye  miradi  mliyoomba ili  ziweze kuwa  na thamani kubwa  kwa kulinganisha  na  masuala yatakayojadiliwa  kwenye  mkutano huu”, Alisema  Sungura

Kwenye  mkutano  huo   mada  mbalimbali  zitawakilishwa ikiwemo  usalama wa Mwandishi  na  vifaa  vyake, kuripoti  habari za kitakwimu,  migogoro inayochochewa  na  rasilimali  za  Afrika, pia   kutakuwa  na  mada  zitakazowasilishwa  na mabingwa  wa  habari  za uchokonozi  kama  Mohammed Ally , Mwandishi  anayetoka kituo  cha  luninga  cha  KTN.

Tanzania  imewakilishwa  na  Waandishi  wanne  chini  ya  ufadhili  wa  TMF, ambao  ni  Veronika  Mataba  (Radio  Faraja), Edwin Soko (Redio  SAUT  FM), Irene  Mbakilwa(TBC  Iringa), na  Nicholas  Ngaiza(Radio  Kasibante  Kagera)
Chi  ishirini  na  mbili zinahudhuria  mkutano  huo.

Wakiongea  kwa  pamoja  wameahidi  kujifunza  mengi  yatakayoweza  kuisaidia  Tasnia  ya  habari  Tanzania  ili  kuchangia  kwenye  kukuza  maendeleo  ya Nchi  kwa kuzingatia   msingi  mkubwa wa  ukweli  kwenye  uandishi wa habari.

Wakati  huo    Waandishi wa  Kenya  wameutaja  muswada  wa  sheria  ya  vyombo  vya  habari  ulipitishwa  na  bunge    hivi  karibunu  kuwa ni  muswada mbaya  sana  ambao  unadhoofisha  taasnia  ya  habari  Tanzania.

“Nimusoma  muswada  huo  naona  ni mbaya  kuliko katika  ukanda  wa Nchi za Afrika  ya  mashariki, pia  nahisi  kwa  sasa  kuna  ajenda  ya  Afrika ya  Mashariki  kuviminya  vyombo  vya  habari” Alisema  Mwandshi  John  Allan  toka standard   Group  ya  Kenya”

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.