ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 6, 2016

WALIMU WA SAYANSI NI TATIZO MWANZA.

Halmashauri ya Jiji la Mwanza inakabiliwa na upungufu wa walimu 296 wa masomo ya sayansi na 41 wa sanaa katika shule za Sekondari za Serikali.
Ofisa Elimu Sekondari wa jiji hilo, Joseph Gwasa alitoa taarifa hiyo wiki iliyopita akisema upungufu wa walimu hao wa sayansi ni sawa na asilimia 52 na wa sanaa ni asilimia 4.4 ya mahitaji.

“Hadi sasa tuna walimu 274 wa masomo ya sayansi, wakati mahitaji ni walimu 570 kwenye sekondari zote 30 za umma ndani ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza, masomo ya sanaa tunahitaji walimu 41,” alisema Gwasa.

Amefafanua kuwa halmashauri hiyo  ina walimu 878 wa sanaa.

Mmoja wa walimu wa Shule ya Sekondari ya Mapango ambaye hakutaka kutajwa jina lake, alisema licha ya baadhi ya sekondari kukabiliwa na upungufu wa walimu wa  sayansi, wanafunzi wengi wanaofaulu kuendelea na kidato cha tano wanatoka mchepuo huo.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Kiomoni Kibamba amesema ofisi yake inaendelea kukabiliana na changamoto za upungufu wa walimu wa sayansi.

Vilevile, amesema wanahamasisha wanafunzi  kusoma masomo ya sayansi na kuondokana na dhana kuwa ni magumu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.