ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 11, 2017

SASA NI RASMI FAINALI YA UEFA:- JUVENTUS KUKIPUTA DHIDI YA REAL MADRID


Hakuna siri tena baada ya fumbo kufumbuliwa, ni wazi sasa tena rasmi fainali ya UEFA Champions League 2017 inakwenda kuwakutanisha Kibibi kizee cha Turin Juventus dhidi ya Real Madrid.

Juventus kwa mara ya pili imefuzu katika fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya baada ya kuishinda Monaco kwa jumla ya mabao 4-1

Juventus ambao hawajashinda kombe hilo tangu 1996 na waliopoteza katika fainali ya mwaka 2015 dhidi ya Barcelona watakabiliana na Real Madrid walioshinda leo kwa jumla ya mabao 2-4, katika uwanja wa Cardiff mnamo tarehe 3 mwezi Juni.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.