ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 15, 2017

MAHAFALI YA PILI NA TATU YA KIDATO CHA SITA WAJA SEKONDARI YAFANA MKOANI GEITA

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya  WAJA  wakiwa kwenye msafara wa kuingia ukumbini kwaajili ya sherehe za kupongezwa kuhitimu kidato cha sita.

Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Geita pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya WAJA  Mhandisi Chacha Mwita akiwa na meneja wa shule hiyo wakiingia kwenye viwanja kwaajili ya kukagua Gwaride la Vijana wa Skauti 

Mkuu wa Wilaya ya Geita akikagua kikosi cha Skauti pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya WAJA.

Vijana wa Skauti wakipita mbele ya Mgeni Rasmi  kwa mwendo Kasi.

Mgeni Rasmi pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi za WAJA wakishuhudia Gwaride la Vijana wa Skauti.

Mkurugenzi wa Taasisi za WAJA Mhandisi Chacha  Mwita wakiteta jambo na Mgeni Rasmi  Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi wakati wa mahafali ya shule hizo.


Msafara ukiingia kwenye ukumbi wa sherehe za mahafali.

Wahitimu wa Kidato cha Sita shule ya Sekondari ya Wasichana na Wavulana ya WAJA.

Mshehereshaji MC  Foka foka akiwakaribisha wageni waalikwa pamoja na wanafunzi wa Kidato cha Sita.

Meza kuu ikigonga chance ishara ya upendo na amani.

Mkurugenzi wa Taasisi za WAJA ,Mhandisi  Chacha Mwita akitambulisha na kuzungumza na  wagenu waalikwa pamoja na wazazi na walenzi  ambao waliuzulia  hafra ya kuwapongeza wanafunzi wa Kidato cha Sita.

Wageni waalikwa na wazazi.

Mchezo wa sarakasi ukiendelea kwenye ukumbi wa sherehe hizo.

Meneja wa Taasisi za WAJA,Bi Jackline Tesha akitoa salaam  kwa niaba ya wafanyakazi wa WAJA.

Mkurugenzi wa Taasisi za WAJA ,Mhandisi  Chacha Mwita akitambulisha na kuzungumza na  wagenu waalikwa pamoja na wazazi na walenzi  ambao waliuzulia  hafra ya kuwapongeza wanafunzi wa Kidato cha Sita.

Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akizungumza na wanafunzi,Wazazi na wageni waalikwa kwenye mahafali ya  kidato cha Sita.





Mgeni Rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa WAJA.

Wahitimu wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni Rasmi.



PICHA NA JOEL MADUKA WA MADUKA ONLINE

Shule ya Sekondari ya wavulana na wasichana ya WAJA imefanya mahafali ya Kidato cha sita leo ambapo kwa upande wa Wasichana ni Mahafali  ya Tatu na kwa wavulana ni ya Pili tangu kuanza kwa Kidato cha Tano na cha Sita.

Jumla ya wahitimu 113 wamehitimu  ambapo kwa upande wa shule ya wasichana ni wanafunzi 79 na wavulana ni 34 ambapo ni katika michepuo ya sayansi na Sanaa.

Mafanikio ambayo yameweza kupatikana katika shule zote mbili ni kutokana na kuwepo kwa taaluma ambayo inamwandaa mwanafunzi kuwa na uwezo wa kujitegemea ambapo katika mitihani ya kanda ya ziwa shule ya wasichana ya WAJA Girls ilishika nafasi ya 19 kikanda kati ya shule 57 na huku ikiwa ya tatu kati ya shule 11 Mkoani Geita.

Kwa upande wa shule ya Wavulana ya WAJA ilishika nafasi ya 20 kikanda kati ya shule 57 huku wakishika nafasi ya 4  kati ya shule 11 zilizopo Mkoani Humo.

Hata hivyo kwa upande wa michezo shule Hizo zimeendelea kufanya vizuri hali ambayo imesababisha kuboresha viwanja vya michezo .

Akihutubia Wanafunzi Kwenye Maafari hayo Mkuu wa Wilaya ya Geita ambaye alikuwa ni Mgeni Rasmi Mwl,Herman Kapufi amewasisitiza wanafunzi kuwa na mienendo ambayo ni mizuri pindi watakapo kuwa kwenye jamii zinazo wazunguka na kuachana na tabia zinazoweza kuwasababishia kutokutimiza ndoto ambazo wamejiwekea.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Taasisi za WAJA ambazo zinamiliki shule hizo,Mhandisi Chacha Mwita ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kupunguza Tozo ambazo zinaonekana kuwa zinawakandamiza kama za vibao vya shule ambazo zinaonesha sehemu ambayo shule inapatikana pamoja na swala la majengo ambayo yamekuwa yakitozwa Fedha nyingi tofauti na matarajio ambayo wao wanafanya shughuli zao ambapo kwa mwaka unakuta kodi wanalipa kiasi cha sh,Milion 12 .

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.