ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 13, 2017

WAKAZI WA MABONDENI UKONGA WATAKIWA KUHAMA MAENEO HAYO.

WAKAZI wa ukonga waishio kwenye maeneo yasiyo salama kama vile mabondeni wametakiwa kuhama mara moja kwenye maeneo hayo na kuacha kushindana na Serikali.
Wito huo umetolewa na Mbunge wa Ukonga jijini Dar es salaam, Mwita Waitara wakato alipowatembelea wakazi wa kata nne zilizokumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia mvua zilizonyesha jijini humo.

Mbunge huyo aliwapelekea misaada mbalimbali wananchi walioathirika kutokana na mafuriko yaliyoletwa an mvua hizo.

Aidha, kwa upande wao wananchi waliokumbwa na maafa hayo walimshukuru mbunge wao ikiwa ni pamoja na kuzungumzia changamoto zinazowakabili.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.