ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, February 7, 2017

MAKALA:-  YAJUE MAADILI YA MADIWANI.


MAKALA

 YAJUE MAADILI YA MADIWANI

Na James Timber, Mwanza

Kanuni za Serikali za Mitaa, Mamlaka za Miji kuhusu Maadili ya Madiwani za mwaka 2000 ambapo Kanuni hizi zimeundwa chini ya Sheria za Serikali za Mitaa na Mamlaka za Wilaya ya Mwaka 1982.

Nini maana ya Diwani?, Diwani ni Mjumbe wa Halmashauri anayofanyia kazi.

 Misimamo ya msingi, Kaulimbiu, Majukumu na Malengo.

Kaulimbiu,  Diwani atatakiwa kuzingatia kaulimbiu ya Halmashauri inayoendesha shughuli zake kwa misingi ya demokrasia na inayotekeleza majukumu yake kwa ufanisi, uaminifu, udhibiti na kwa namna inayowajali wananchi wake.

Jukumu la msingi, Diwani kwa kushirikiana na madiwani wenzake, watumishi wa Halmashauri wa Umma kwa ujumla watafanya kazi kwa lengo la kuhamasisha maendeleo endelevu ya kiuchumi katika Kata yake na Katika eneo la Halmashauri.

Lengo, Lengo la Kanuni hizi za Maadili ni kufafanua Taratibu za Mwenendo wa Madiwani utakaowawezesha  kutekeleza majukumu yao kwa namna itakayojenga na kudumisha imani  ya umma kwa serikali zao za Mitaa.

Kanuni za  maadili ya Madiwani, Wakati wote anakuwa na  mwenendo mzuri kwa umma inayoweza  kulinda imani kwa Halmashauri.

Anazingatia Sheria, na kwamba wakati wote matendo yake yanaendana na dhamana aliyopewa na umma.

Diwani anaisaidia Halmashauri kwa kadri iwezekanavyo kuendesha shughuli zake kwa kuzingatia maslahi ya jamii nzima ya Halmashauri ambayo anaifanyia kazi.

Diwani hajiweki katika mazingira ambamo heshima na utu wake unatiliwa mashaka.

Aidha Diwani anawajibika kwa wapiga kura wake na jamii yote ya Halmashauri kwa matendo yake na kwa maamuzi yatakayofanywa na Halmashauri, kwamba Diwani anakuwa muwazi katika matendo yake na kuyaelewa maamuzi ya Halmashauri na kuyasimamia.

Diwani lazima afanye maamuzi bila ya upendeleo na bila kushawishiwa na mawazo ya watu wengine hasa anapotekeleza shughuli za umma, na anaposhiriki uteuzi  wa watumishi wa umma wakati wa kutoa mikataba au wakati wa kutoa mapendekezo ya kutoa zawadi.

Diwani atatunza siri,  au taarifa atakazopata zinazohusu watu binafsi zinazoshughulikiwa kwa kwa mujibu wa sheria au kwa manufaa ya umma na hazitumiki kwa shughuli zake binafsi.

Marufuku kutangaza maslahi yoyote ya binafsi yanayohusiana na utendaji wake wa shughuli za umma wakati wa mkutano wa Halmashauri au wa Kamati ambayo yeye ni mjumbe.

Na mwisho Diwani ataheshimu nafasi ya watumishi wa umma na Maofisa wa Halmahauri anayofanyia kazi kama mjumbe, na kuwatendea namna ambayo inajenga heshima kwa pande zote.

Vigezo vya tabia binafsi, Kila Diwani atatakiwa;

Kuwa mtenda haki, muwazi, mkweli, mwaminifu kitaaluma na kisiasa na asiwe na migongano ya kimaslahi.

Kuendesha maisha yake kwa namna itakayolinda heshima ya Halmashauri na kuinua imani ya  umma kwa Halmashauri.

Kwa madhumuni ya kuinua au kuongeza imani ya umma, Diwani anatakiwa kuzingatia kiwango cha juu  kabisa cha uadilifu wakati anapokuwa Diwani.

Diwani hatakuwa na uhusiano usioruhusiwa wa kimapenzi na Diwani mwenzake au mtumishi wa Halmashauri.

Madeni na marafiki, Diwani hatakiwi kutumia vibaya dhamana na imani aliyonayo kwa umma kama,

(a) kukopa kwa kiwango kinachozidi uwezo wake wa kulipa madeni yake au kwa kiwango ambacho kinamwondolea hadhi au kudhoofisha uwezo wake wa kutenda na kufanya maamuzi yenye msimamo,

 (b) kuwa na uhusiano na watu na tabia zenye mashaka kwa namna inayoharibu mtazamo na imani waliyonao kwa Halmashauri.

charitytimberland@gmail.com

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.