ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 9, 2016

TIGO SASA YATAMBA MWANZA NA 4G LTE.

Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Ally Maswanya (katikati) akiwaongoza wadau wenzake wa Kampuni ya Mawasiliano Tigo, Edgar Mapande ambaye ni Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa (kulia) na Benedict Mponzi ambaye ni Meneja wa Mtandao wenye kasi zaidi katika kuperuzi na kupakua kwa urahisi kutoka kwenye mtandao wa intaneti wa 4G , katika utoaji taarifa ya uzinduzi wa 4G uliofanyika ndani ya Hotel Gold Crest Jijini Mwanza.
Wateja wa waishio Mwanza sasa wanaweza kupata mtandao wa internet wenye kasi kubwa zaidi kufuatia upanuzi wa upatikanaji wa huduma ya 4G LTE hadi kufikia jiji hilo linalopakana na Ziwa Victoria nchini Tanzania, Teknolojiaya 4G LET ina kasi mara tano zaidi kuliko teknolojia ya 3G inayopatikana nchini kwa sasa. ZAIDI BOFYA PLAY.

"Upanuzi huu umetokana na mafanikiomakubwa yaliyopatikana katika majaribio ya awali ya utoaji huduma ya 4G jijini Dar es salaam kuanzia mapema mwaka jana". amesema Mkurugenzi wa Kanda ya Ziwa, Ally Maswanya. (kulia), akiwa na Meneja wa 4G Benedict Mponzi.
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Ally Maswanya (katikati) akikazia jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya huduma mpya Kanda ya Ziwa. Kulia ni Bw.  Edgar Mapande ambaye ni Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa na Benedict Mponzi ambaye ni Meneja wa Mtandao intaneti wa 4G , Mtandao wenye kasi katika utoaji taarifa ambao sasa rasmi Jijini Mwanza.
Card ya 4G ambayo kila mteja wa Tigo atakaye taka kuifaidi huduma hiyo atapaswa kubadilishiwa ile yake ya zamani na kuipata hii yenye vihusishi vya teknolojia hiyo ya kisasa na yenye kasi zaidi.
Wanahabari kikazi zaidi.
Kuhusu namna ya kujiunga na jinsi ya upatikanaji wa huduma hiyo Meneja wa 4G Benedict Mponzi anafunguka zaidi. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.


Wateja wote wa Tigo 4G LTE watanufaika na promosheni: Kila atakapoongeza salio la shilingi elfu moja au zaidi atapata MB 500 bure kama bonasi.
Wanahabari walipata wasaa wa kuuliza maswali.
Wateja wa waishio Mwanza sasa wanaweza kupata mtandao wa internet wenye kasi kubwa zaidi kufuatia upanuzi wa upatikanaji wa huduma ya 4G LTE hadi kufikia jiji hilo linalopakana na Ziwa Victoria nchini Tnzania, Teknolojiaya 4G LET ina kasi mara tano zaidi kuliko teknolojia ya 3G inayopatikana nchini kwa sasa.
Edgar Mapande Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa.
Tunaposema ni muda wa kubadili kutoka 3G kwenda 4G jeh hii inamaana kuwa mtu akibadili na kuwa ndani ya simu card yenye uwezo wa 4G hatoweza kupata mawasiliano pindi atakapo kwenda eneo lenye 3G, na vipi huduma hiini ya manufaa kwa watu wa mijini tu, vipi wadau maeneo ya ndani vijijini. BOFYA KUSIKIA MAJIBU YA SWALI LA WENGI. 

Kulia ni Edgar Mapande ambaye ni Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa akijibu maswali kusanyikoni, pembeni yake Mkurugenzi wa Tigo Kanda Ally Maswanya.
Jiografia ya kusanyiko hilo.
Tigo.
Vipi mteja atatozwa gharama yoyote katika kuhama mtandao wa 3G kwenda 4G?
Na vipi muda wa kuhama hasa ukizingatia wingi wa wateja ninyi kama Tigo mtawezaje kuwamudu kwa kasi inayohitajika hamuonikwamba huu utakuwa usumbufu mpya kwa wateja wenu?BOFYA PLAY KUSIKILIZA MAJIBU.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.