ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 20, 2014

HIZI HAPA PICHA ZA TAMASHA SERENGETI FIESTA LILILOPIGWA JIJINI DAR

Majina yote mpe yeye,mara Dangote,mara Chibu afu jazia na Diamond Platnum akiwa kazini na skwadi lake zima la kazi alipiga Bo..bo...bonge la Show Fiestani 2014.
Msanii wa muziki kizazi kipya,Rachael kutoka THT akitumbuiza jukwaani kwenye usiku wa tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika katika viwanja lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.
Sehemu ya  umati wa watu waliokuwa wakishuhudia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la Fiesta 2014 katika viwanja vya Lidaz Kinondoni jijini Dar.
Mmoja wa wasanii wa kike wanaofanya vyema katika anga ya muziki wa Bongogfleva,Shah akiwa na skwadi lake wakilishambulia jukwaa la fiesta.
Mkali mwingine wa steji,ambae amekuwa akifanya vyema kwenye matamasha mbalimbali ya fiesta,ukipenda muite Kabyser ama Mr Blue akiimba jukwaani mbele ya umati wa watu waliofika kwenye tamasha la Fiesta 2014,ndani ya viwanja vya lidaz club jijini Dar
Mkali mwingine wa hip hop nchini Mwana-FA akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo pichani) usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la Fiesta 2014.
Kama kawaida yao wawapo jukwaani,ni kushambulia jukwaa mwanzo mwisho,pichani kulia ni Stamina na Ney wa Mitego wakikamua jukwaani.
Abdulkiba nae akionesha yake jukwaani.
Ilikuwa ni shoo moja nzuri kutoka nyumba ya vipaji ya THT.
Ilikuwa buruuudani kabisa.
Pichani msanii Linah (nyeupe) akiwa na skwadi lake mara baada kumaliza kulishambulia jukwaa kwa pamoja.
Anaitwa Ally kiba ambaye inaelezwa kutoka kwa mashabiki  kuwa alifanyo shoo nzuri na iliyowavutia,na kuthibitisha uwezo wake kuwa ni kweli amerejea kwenye kiti chake cha usanii.
Mashabiki wakifuatilia tamasha la Fiesta 2013.
Msanii kutoka nchini Marekani Clifford Haris a.k.a T.I akiwasili kwenye viwanja vya lidaz club Kinondoni jijini Dar kutumbuiza tamasha la Fiesta lililofanyikamwishoni mwa wiki.
Msanii kutoka nchini Nigeria, David Adedeji Adeleke a.k.a Davido akiwakuna mashabiki wake kwa kucheza staili yake ya Skelewi jukwaani,huku miluzi na shangwe ikiwa imetawala kila kona ya uwanja.
Davido na Diamond wakilishambulia jukwaa kwa paoja.
Davido na Diamond.
Skelewu ya Davido na Ngololo ya Diamond.
Msanii kutoka nchini Marekani Clifford Haris a.k.a T.I akilishambulia jukwaa la Fiesta vilivyo.
 NO MEDIOCRE
Mashabiki toka mataifa yote nao walishangweka kwa raha zao
T.I akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo pichani ) na wimbo wake wa NO MEDIOCRE.
Pichani juu na chini ni sehemu ya umati wa watu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha fiesta usiku wa mwishoni mwa wiki, katika viwanja vya Lidaz Kinondoni jijini Dar.
 Lidaz Kinondoni jijini Dar.
Ilikuwa ni sheeeddddaaa.
Ni Shedah....
Shaha na skwadi lake wakilishambulia jukwaa.
Ommy Dimpoz na Victoria Kimani wakilishambulia jukwaa la fiesta 2014
Palikuwa hapatoshi.
Victoria Kimani akilishambulia jukwaa
Palikuwa hapatoshi jukwaani kwa kila aina ya burudani
Mmoja wa askari waliokuwa wamepangwa katika suala zima la kusimamia usalama ndani ya tamasha la Fiesta 2014 akihakikisha usalama wa kutosha unakuwepo katika eneo hilo,na watazamaji wanapata burudani iliyokusudiwa kutoka kwa wasanii mbalimbali waliotumbuiza usiku wa mwishoni mwa wiki.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.