ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 22, 2014

WATU 115 WALIFARIKI KATIKA KANISA LA T.B. JOSHUA

 Serikali ya Afrika Kusini inasema kuwa watu miamoja na kumi na tano wengi wao wakiwa raia wa Afrika Kusini, walifariki baada ya kanisa kuporomoka nchini Nigeria.

Idadi kamili ya raia wa Afrika Kusini waliofariki ilikuwa 84.
Ndege iliyowabeba manusura wa mkasa huo, kumi na sita kati yao wakiwa wamejeruhiwa vibaya, imewasili mjini Pretoria.
Zaidi ya watu 300 kutoka Afrika Kusini walikuwa wametembelea kanisa hilo la 'All Nations' mjini Lagos, ambalo linaongozwa na mhubiri T.B. Joshua.
Inaarifiwa jengo hilo liliporomoka kutokana na ujenzi mbovu.
Mhubiri TB Joshua, amezua wasiwasi baada ya kuzungumzia kuona ndege iliyokuwa inazunguka juu ya kanisa hilo kabla ya jengo lenyewe kuporomoka
ZIFUATAZO NI PICHA MBALIMBALI KWA HISANI YA MITANDAO NCHINI NIGERIA
Greda likifanya usaidizi kuondosha kifusi cha jengo la kanisa lilio anguka
Harufu ikiwa imetanda, vumbi zito likiwa limetawala shughuli ni moja tu ufukuaji.
Hapa kinachosakwa ni mtu aliye hai au miili zaidi.
Ni kazi nzito ya kukatisha tamaa.
Wapi pa kuanzia au tuanzie wapi....?!!

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.