ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, April 22, 2014

H. BABA ATEMBELEA NYUMBANI KWAO MAREHEMU JAMES DANDU.

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya H. Baba safari hii katika zama za sikukuu ametumia likizo yake kutembelea nyumbani katika kijiji alichozaliwa marehemu James Dandu, huyu alikuwa ni mmoja kati ya wanamuziki walioitangaza vyema sanaa ya muziki wa kizazi kipya Tanzania na hata kuleta mapinduzi makubwa ya muziki huo likiwemo suala la uchapaji wa Video bora na Ubunifu wa Tuzo za Kilimanjaro.
H. Baba (wa pili kushoto) akiwa na Mzee Dandu mwenyewe (wa kwanza kushoto), wengine ni mama mdogo wa James Dandu na ndugu mwingine katika kijiji cha Ngudu wilayani Kwimba mkoani Mwanza.
Kwa mujibu wa H. Baba anasema kuwa lengo la safari hiyo ni harakati zake kama msanii kujengea moyo wa upendo, ushirikiano na kuthaminiana kwa wasanii ili kudumisha umoja na udugu katika sanaa, ikiwa ni pamoja na kuwaenzi wasanii walio kuwa chachu ya wengine kuwa wanamuziki.
H. Baba anasema kuwa ilikuwa ndoto yake ya kipindi kirefu kufika mahali alipozaliwa Marehemu James Dandu, ikiwa ni pamoja na kufika mahala alipozikwa kwani msanii huyo wakati akifariki dunia H. Baba alikuwa anasoma na uwezo wa kufika eneo la mazishi ilikuwa utata enzi hizo sasa kiu aliyokuwa nayo imetimia kwa kupata faraja ya kufika alikozaliwa na kuzikwa mtu aliyemvutia katika sanaa.
James Dandu kuzaliwa 5/07/1970 na kufariki 27/08/2002.
H. Baba akiwa na baadhi ya wajukuu wa Mzee Dandu alioambatana nao katika shughuli ya kupalilia kaburi la James Dandu.
PIcha ya pamoja.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.