ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 22, 2013

AIRTEL YAZINDUA GHARAMA NAFUU ZA KUPIGA SIMU MITANDAO MINGINE.




Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano Mallya akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha inayomwenzesha mteja wa Airtel kupata kifurushi cha maongezi, sms na internet na kuwasiliana na mitandao yoyote nchini, huduma hii imebeba ujumbe wa simkadi moja, taifa moja, bei moja.

Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akielezea huduma mpya ya Airtel yatosha yaani Simu kadi moja, taifa moja, bei moja inayomwezeshamteja wa Airtel kuwasiliana na mitandao yoyote nchi na kupata kifurushi cha muda wa maongezi, sms, na internet kwa bei nafuu hadi shiling 349/= pichani (katikati) ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano Mallya akifatiwa na Meneja masoko Airtel Anethy Muga.




Airtel yazindua gharama nafuu zakupiga simu mitandao mingine
*         Airtel yadhihirisha simu kadi moja, taifa moja, bei moja - Wateja nchini kufaidika na kiwango cha chini cha hadi 75% kupiga simu popote bila kikomo

*          Piga simu muda wowote usiku and mchana

Dar Es Salaam  Jumatano 20 Marchi 2012.  Airtel Tanzania leo imezindua huduma mpya ijulikanayo kama "AIRTEL YATOSHA" itakayowawezesha wateja wake  nchi nzima kupiga simu kwenda mtandao wowote kwa kiwango nafuu cha hadi asilimia 75 bila kuwa na  sababu kubadili simu laini kwa kuhofia gharama.

Huduma ya AIRTEL YATOSHA inadhihirisha simu kadi moja, taifa moja, bei moja  inayoendeleza dhamira ya Airtel ya kutoa huduma bora na nafuu ambapo wateja wa Airtel sasa watapata ofa ya kifurushi kitakacho wapa muda wa maongezi, ujumbe mfupi na kifurushi cha internet ambacho kinaweza kutumika kwa siku au kwa wiki kulingana na mahitaji ya wateja

Akiongea wakati wa hafla maalum ya uzinduzi wa huduma hiyo iliofanyika katika makao makuu ya Airtel Tanzania, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bw Sunil Colaso Alisema"  Huduma ya Airtel YATOSHA ni maalum kwa kila mtanzania, hii itawarahisishia watanzania wote kupata mawasilino nafuu kwa kupiga bila kikomo kwenda mitandao mingine nchini. 

Kupitia kifurushi cha Airtel YATOSHA wateja wa Airtel watafurahia kiwango cha chini cha hadi shilingi 349/=, hii inamaana kwamba  mteja atapata dakika 10 za kupiga simu kwenda mtandao wowote muda wowote, pia SMS 100 (ujumbe mfupi wa maneno) pamoja na kifurushi cha intenet cha 25MB ofa itakayotumika masaa 24 kwa siku

Faida za AIRTEL YATOSHA kwa mteja zinadhihirisha dhamira yetu Airtel ya kutoa huduma za mawasiliano bora na nafuu nchini. Airtel tunazingatia kuwa wateja wetu wanamahitaji tofauti na ndio sababu kubwa inayotufanya tuwe wabunifu kwa kuwapatia huduma zinazogusa kila
aina ya wateja na kuleta mabadiliko halisi kwa kuwapa wateja wetu nchi nzima thamani ya pesa zao

Kwa Upande wake  Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel  Bi,i Beatrice Singano Mallya alisema " Airtel YATOSHA  ni huduma inayopatikana kwa SIKU au kwa WIKI hivyo mteja anapewa nafasi ya kuchagua anachokata.
Katika mpango wa WIKI mteja atatozwa shilingi 1,999  na kupata dakika 70, sms 700 na kifurushi cha interneti cha 175MB.

Kujiunga na huduma hii mteja anatakia kupiga *149*99#  na kuunganisha moja kwa moja kwenye orodha ya huduma hii na kuchangua kifurushi anachokipenda na kuweza kujipatia dakika za maongezi, ujumbe mfupi na kifurushi cha internet.  Dakika za maongezi zitatumika kupiga simu kwenda mtando wowote nchini kwa massa 24 na gharama za kupiga simu
zitatozwa kwa sekunde.

Kuhusu muda wa kujiunga na Airtel YATOSHA mteja anaweza kujiunga wakati wowote  kati ya 0500hrs to 2359hrs,

Airtel Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma zenye ubora na ubunifu nchini. Na hii ni njia nyingine ya kudhihirisha jinsi Airtel inavyotoa huduma za mawasiliano yenye ubora na gharama za ushindani kwa watanzania. Airtel itaendelea kuwa chachu ya maendeleo
kwa kutoa huduma  bora zenye gharama nafuu.

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. Big up kwa taswira za Mwanza.
    Mdau, Dirty South.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.