ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 29, 2012

KALAMA NYILAWILA FRANSIC CHEKA USO KWA USO LEO JUMAMOSI


Na. Super D Boxing Coach

Francis Cheka
MIAMBA ya masumbwi nchini, bingwa wa Mabara Francis Cheka [SMG] na aliyekuwa bingwa wa Dunia Karama Nyilawila [Kapten] wanatarajia kupanda ulingoni leo tarehe 29/09/2012 kuoneshana umwamba.

Cheka na Nyilawila walitwangana mbambanmo wao uliofanyika morogoro ata hivyo ulizua utata baada ya mpambano wao kugubikwa na alama za mshangao ambalo cheka aliibuka na ushindi wa point  mashabiki kuhisika wa mabondia hao wanaogopana na kutafutana kwa mda mrefu watapoza kiu yao kwa mpambano huo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, promota wa pambano hilo Oswald Mlay alisema pambano hilo litapigwa katika uwanja wa PTA Sabasaba
.
Alisema pambano hilo litakuwa la raundi 12 uzito wa kg 72 ambapo leo wamepima uzito kwa ajili ya mpambano huo utakaoamua nani zaidi

Katika Mchezo huo kutakua na Uhuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.