ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 11, 2018

MWENYEKITI UVCCM AFIKA KUHANI NYUMBANI KWA DIWANI ALIYEFARIKI KWENYE AJALI

 Mwenyekiti wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM) na Mjumbe wa Kamati Kuu (MCC) Comred Kheri James leo mchana amefika Nyumbani kwa Familia ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Tindabuligi Marehemu  Mahega Masunga Seleman kwa ajili ya kuhani msiba na kutoa Mkono wa pole kwa Familia, Mjane, Wananzengo,  Ndugu, Jamaa, wanaWananchi wa Kata ya Tindabuligi na wanaCCM wa Wilaya Meatu.


Mwenyekiti aliambatana na Mhe Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki na  Naibu Waziri wa Madini Stanislaus Nyongo, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu,   Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mwenyekiti wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Simiyu Ndugu Lumen Mathias, Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa Bi. Rose Manumba, Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa Shaban Kiduta na wajumbe wa Kamati za Siasa Mkoa na Wilaya.

Mwisho, Mwenyekiti wa Vijana Taifa amewaomba Watanzania kuendelea kuwaombea Majeruhi wa Ajali ambao Mchana wa leo wamesafirishwa kwenda Hospitali ya Taifa ya Mhimbili kitengo cha Mifupa (MOI).
Lumen Mathias.

Mwenyekiti wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Simiyu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.