ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 26, 2017

BASI LATEKETEA KWA MOTO MKOANI TANGA.

Basi aina ya Yutong iliyokuwa ikitoka Tanga mjini kuelekea Dar es salaam, limeungua moto maeneo ya Pongwe karibu na mizani majira ya saa 8: 30 mchana wa leo.

Kwamujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi Benedict Michael Wakuyamba amesema basi hilo lenye namba za usajili T T361 DCF limewaka moto katika eneo la Pongwe jiji Tanga, na hakuna madhara yoyote kwa binadamu zaidi ni hasara ya mizigo ilikuwa imewekwa kwenye buti.

Basi hilo liliokuwa likiendeshwa na dereva  Hemedi Ali (35) mkazi wa Tanga lilikuwa likitokea Tanga kuelekea jijini Dar es salaam likiwa limebeba abiria 29 lilipofika eneo hilo liliwaka moto

 Kamanda Benedict amesema kwamujibu maelezo ya awali ya Dereva huyo anadai alianza kuhisi paipu ya gari inawaka  na ndipo aliposimamisha gari hilo, Mpaka sasa Jeshi hilo bado linaendelea kumuhoji dereva huyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.