ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 9, 2017

KENYA: POLISI WATAWANYA WATU WANAOCHOMA MATAIRI.

NAIROBI. Jeshi la Polisi katika Mji wa Kisumu, nchini Kenya limelazimika kuanza kutumia nguvu kuwatawanya kundi la vijana waliojitokeza mtaani kuanza kuchoma matairi ya magari, wakidai kuibiwa kura kwa mgombea wao wa urais anayeungwa mkono na Muungano wa Nasa, Raila Odinga.

Tukio hilo limetokea baada ya saa chache Odinga kujitokeza mbele ya vyombo vya habari akituhumu uchakachuaji wa kura zake uliofanywa na Tume ya Uchaguzi isiyokuwa na mipaka (IEBC) wakati wa tukio la kuhesabu kura.

Wananchi nchini Kenya walipiga kura katika Uchaguzi Mkuu siku ya jana ,kabla ya vituo hiyo kufungwa kuanzia saa 11:00 jioni.

Mwandishi wetu aliyeko nchini Kenya, Noor Shija ameshuhudia vurugu hizo zikiendelea katika maeneo ya mitaa ya Kisumu hatua iliyosababisha kufungwa kwa baadhi ya barabara ya Kasumu Kakamea. Polisi walilazimika kutumia nguvu huku wakirusha risasi hewani ili kuwatawanya.

Baadaye Polisi iliamua kuondoa mawe yaliyokuwa yametegwa na vijana hao barabarani.Katika hatua nyingine, kuna taarifa za kupigana kwa wafuasi wa wagombea ubunge katika kituo vha kujumlishia matokeo , kilichopo Mji wa Mokewe, uliopo Lamu kabla ya Polisi kuwasili eneo la tukio na kurejesha hali ya utulivu

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.