ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 10, 2017

WAPINZANI WAMTAKA MUGABE AJIUZULU, WASEMA ANAIONGOZA NCHI AKIWA KITANDANI HOSPITALI.


Vyama vya upinzani nchini Zimbabwe vimerejea wito wao wa kutaka Rais Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 93 ajiuzulu, na kumlaumu kwa kuiongoza nchi kutoka hospitalini.
Taarifa ya wapinzani wa Zimbabwe imeeleza kuwa, Mugabe hana uwezo na nguvu za kuiongoza tena nchi hiyo hasa kutokana na kuwa hospitali mara kwa mara.

Gazeti la binfasi la News Zimbabwe limenukuu Obart Gutu, msemaji wa chama kikuu cha upinzani cha MDC akisema kuwa, Mugabe ni lazima aondoke na aiache Zimbabwe kusonga mbele chini ya uongozi mpya. Ameongeza kuwa, hawezi kuiongoza nchi akiwa kitandani hospitalini.

Karauone Chihwayi, msemaji wa upande wa tawi lilijitoa ndani ya MDC naye ametoa matamshi kama hayo.  Amebainisha kama ninavyomnukuu: Nchi hii imekwama kwa sababu rais wa ZANU-PF anaongoza akiwa katika kitanda cha hospitali."

Rais Ribert Mugabe wa Zimbabwe.

Wito wa wapinzani wa  kumtaka Rais Mugabe ajiuzulu umekuja masaa machache baada ya kuripotiwa kwamba, kiongozi huyo wa Zimbabwe yuko nchini Singapore kwa ajili ya matibabu, hii ikiwa ni safari yake ya tatu ya kitiba nchini humo mwaka huu.
 
Pamoja na kuwepo wasiwasi kuhusu hali yake ya afya, Mugabe amesafiri mara 10 nje ya nchi mwaka huu na safari yake ya mwisho ya kikazi ilikuwa wiki iliyopita wakati alipohudhuria kikao cha viongozi wa Afrika huko Addis Ababa Ethiopia. Mugabe ambaye ameitawala Zimbabwe tokea ijinyakulie uhuru kutoka Uingereza mwaka 1980 anasema atagombea tena urais mwaka 2018.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.