ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 11, 2017

SUDAN YAFUNGIWA RASMI MABINGWA AFRIKA.

 Timu mbili za Sudan zimetolewa nje ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kupanga ratiba ya robo fainali bila kuzihusisha timu hizo kutokana na uamuzi wa FIFA kuifungia nchi hiyo.

Hatua hiyo imetokana na serikali ya nchi hiyo kuingilia masuala ya soka hivi karibuni ambapo ni kinyume na sheria za Shirikisho hilo.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na CAF, timu ya El Merreikh na Al Hilal Omdurman zilizokuwa Kundi A zimewekwa kando huku michuano ya robo fainali inatarajiwa kukuwakutanisha Al Ahli Tripoli dhidi ya Esperance, Ferroviario da Beira imepangwa na USM Alger, Al Ahly itakutana na Etoile du Sahel wakati mabingwa watetezi Mamelodi Sundowns FC wakipangwa kuanzia nyumbani dhidi ya Wydad Casablanca kutokana na droo iliyochezeshwa na CAF.
Ratiba ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika iliyotolewa na CAF kupitia ukurasa wake wa twitter.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mechi za robo fainali zitapigwa mwezi Septemba, nusu fainali itakuwa Oktoba na fainali itapigwa mwezi Novemba mwaka huu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.