ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 21, 2017

MAMBO 10 ALIYOSEMA RAIS MAGUFULI LEO JULAI 21, 2017 KIGOMA.

Kutokea mkoani Kigoma leo July 21, 2017 amefanya ziara yake ya kikazi ikiwa ni pamoja na kuzindua mradi wa barabara ya Nyakanazi – Kibondo pamoja na Kidahwe – Kasulu, Rais Magufuli amezungumza mambo mengi kwenye hotuba yake ikiwemo kodi, barabara, alivyojitoa kwa Tanzania na mengine.

"Tumeibiwa sana madini, tumewaita waje tuzungumze wakichelewachelewa nitafunga migodi yote, mara kumi wapewe Watanzania" - JPM 

'Kuanzia tarehe 1 mwezi wa 7, 2017 ukibeba mazao hautatozwa ushuru sio kwa gunia tu, hata tani 1 ya gari'' -Rais Magufuli

'Nataka ifike wakati mtu atoke hapa Nyakanazi hadi Dar es Salaam kwa bajaji kwenye lami na hili linawezekana kabisa' - Rais Magufuli

'Nilipokea malalamiko ujenzi unakwenda taratibu mkandarasi asinijaribu, mimi kufukuza makandarasi ni kama kunywa chai'' - Rais Magufuli

''Niwambie ukweli, fedha nyingi zinapotelea serikalini, ndiomana nimezuia semina, posho za ajabu, safari hadi nikupe kibali'' - Rais Magufuli

''Tulipoingia tulikuwa tunakusanya kodi bilioni 800 tukabana tukapata trilioni 1.3, tukibana zaidi tutapata hadi trilioni 3'' -Rais Magufuli

''Tumeondoa tozo katika sekta za mifugo, uvuvi na kilimo ili kutimiza ahadi ya kuwatumikia wananchi'' - Rais Magufuli

''Na nyinyi wananchi msinyamaze, toeni ushirikiano kuondoa tatizo la ujambazi'' - Rais Magufuli

''Mkandarasi fanya kazi usiku na mchana barabara hii ya Kibondo - Nyakanazi ikamilike kwa haraka'' - Rais Magufuli

''Waziri wa Fedha hakikisha mkandarasi analipwa haraka ili tumalize mradi huu haraka iwezekanavyo' -Rais Magufuli

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.