Blogger G. Sengo katika mnara wa kupinga mauaji na vitendo viovu dhidi ya albino wilayani Sengerema mkoani Mwanza, mahala ambako bado vita inapiganwa. |
IKIWA leo ni july 13 mwaka 2017, dunia huadhimisha Siku ya walemavu wa ngozi (albino), mkoa wa njombe umeendelea kuweka
vipaumbele mbali mbali ikiwemo usalama kwa walemavu ili waweze
kutimiza ndoto zao.
Hayo
yamebainishwa na TERESIA YOMO afisa ustawi wa jamii mkoa wa Njombe
ofisini kwake alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari na kuongeza
kuwa kundi hili maalumu wameendelea kuishi vizuri kutokana na utaratibu
ambao huchukuliwa na serikali.
BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
Katika
hatua nyingine afisa huyo wa ustawi wa jamii amebainisha changamoto ya
usafili kutokana na mazingira ya mkoa wakati wanapohitaji huduma za
kiafya, hivyo ametoa wito kwa jamii kuweza kutoa msaada kwa kundi hilo
pindi msaada unapohitajika.
Nao
baadhi ya wananchi wa mtaa wa sido wamesema kuwa ni vema kila mwananchi
kuto kuwa na dhana potofu dhidi yao badala yake kuwe na ushirikiano
katika shughuli za maendelo kwa kuwa ni binaadamu kama wengine.
Mnamo mwezi mei 2017 Tanzania na Umoja wa Ulaya (EU) zilizindua mradi maalumu wa kulinda na
kutetea haki za wazee na watu wenye ualbino katika wilaya
nne zinazoongoza kwa mauaji ya makundi hayo ya jamii Kanda ya Ziwa, Mradi utakao tekelezwa kwa muda wa kipindi cha miaka miwili (2017 – 2019)
katika wilaya ya Misungwi iliyopo mkoani Mwanza, Chato (Geita),
Nzega (Tabora) na Kishapu (Shinyanga).
Na wilaya hizo ndizo zinazotajwa kuwa zinaongoza kwa matukio ya ukatili na mauaji dhidi ya wazee na albino katika kanda hiyo.
Kadhalika, takwimu za kutoka mwaka 2006 zinaonyesha kuwa Albino 74 wameshauawa kikatili, huku 56 wakinusurika kifo, na kati yao 11 wameongezewa ulemavu mwingine wa kudumu.
Na wilaya hizo ndizo zinazotajwa kuwa zinaongoza kwa matukio ya ukatili na mauaji dhidi ya wazee na albino katika kanda hiyo.
Kadhalika, takwimu za kutoka mwaka 2006 zinaonyesha kuwa Albino 74 wameshauawa kikatili, huku 56 wakinusurika kifo, na kati yao 11 wameongezewa ulemavu mwingine wa kudumu.
Kitaifa
maadhimisho haya hii leo yanafanyika mkoani Dodoma ambapo Mkoa wa
Njombe ni miongoni mwa mikoa ambayo ina idadi ndogo ya kundi hilo la
walemavu ambapo serikali imetengeneza utaratibu maalumu wa kutoa kliniki
na matibabu ambayo hutolewa pamoja na vifaa ikiwemo kofia ili kulinda
afya na ngozi zao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.