ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 23, 2017

MAPIGANO MAKALI YARIPOTIWA MASHARIKI MWA CONGO, 16 WAFARIKI DUNIA

Mapigano makali yameripotiwa kati ya askari wa jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na makundi ya waasi huko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo na kusababisha mauaji ya watu 16.

Msemaji wa jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema kuwa, mapigano makali yaliyotokea jana kati ya jeshi hilo na makundi ya wanamgambo katika mji wa Beni mkoani Kivu Kaskazini yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 16 na kujeruhi wengine wengi.

Duru za polisi katika mkoa huo zimeripoti kuwa, mapigano hayo yalitokea wakati waasi walipojaribu kuwaachia huru wafungwa wanaoshikiliwa na vyombo vya usalama.
Maelfu ya watu wameuawa Congo kutokana na machafuko ya ndani.
Maeneo ya mashariki na kaskazini mashariki mwa Congo yamekumbwa na mapigano makali baina ya jeshi la serikali ya nchi hiyo na makundi ya wanamgambo, na maelfu ya watu wameripotiwa kuuawa na mamilioni ya wengine kulazimika kukimbia makazi yao.
 
Uchunguzi uliofanwya na baadhi ya vyombo vya habari umebaini kuwa, watoto wadogo huko katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ndiyo wahanga wakuu wa vita katika vinavyoendelea katika maeneo hayo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.