ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 6, 2017

KIONGOZI WA UPINZANI NIGER AHUKUMIWA KIFUNGO JELA.


Mahakama moja nchini Niger hii leo imetoa hukumu ya kifungo cha miezi mitatu jela dhidi ya kiongozi wa upinzani nchini humo, aliyekuwa akikabiliwa na mashitaka ya kuchochea mapinduzi dhidi ya serikali.
Al-Hadji Amadou Djibo, alikamatwa mwezi uliopita, baada ya kutoa wito kwa wafuasi wake kusimama kidete dhidi ya serikali ya Rais Mahamadou Issoufou.

Hata hivyo wakili wake, Douleur Oumarou, amewaambia waandishi wa habari baada ya hukumu hiyo kwamba wataka rufaa akisisitiza kuwa hukumu hiyo inapania kuwanyamazisha wapinzani na wakosoaji wa serikali.

Kinara huyo wa upinzani wa Niger alitazamiwa kuachiwa huru leo Jumanne toka gerezani.

 
Rais Mahamadou Issoufou wa Niger
Mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu, Mahakama ya Niger iliwaachia huru watu 15 waliokuwa wakikabiliwa na tuhuma za kupanga jaribio la mapinduzi dhidi ya Rais Issoufou wa nchi hiyo. Hata hivyo, wenzao 9 akiwemo anayedaiwa kuwa kinara wa jaribio hilo, Jenerali Salou Souleymane, wangali wanashikiliwa na vyombo vya usalama.
 
Issoufou alichaguliwa tena kuwa Rais wa Niger katika uchaguzi uliofanyika mwezi Februari mwaka jana na kususiwa na kambi ya upinzani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.