ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 30, 2017

JESHI LA POLISI LAUA MAJAMBAZI WANNE KIBITI USIKU WA KUAMKIA LEO.

Jeshi la Polisi limeua Watu wanne wanaozaniwa kuwa ni majambazi kwenye kijiji cha Pagae , Kibiti Mkoani Pwani

Taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari na DCP Lebaratus Sabas Mkuu wa Opereshini Maalumu ya Jeshi hilo Tanzania ambapo amesema kuwa majambazi hao wameuwa jana Majira ya Usiku
kwenye barabara inayotoka Pagae kuelekea Nyambunda.

Taarifa hiyo ya DCP Sabas inasema  kuwa Askari Polisi wakiwa doria walikutana na kikundi cha watu kinachokadiriwa kuwa na watu sita wakitokea barabara kuu ya lami wakifuata barabara hiyo inayoelekea Nyambunda kilomita 100 kutoka barabara kuu.

"Watu hao walipogundua kuwa watu waliokuwa mbele yao ni Askari Polisi  walikimbia vichakani na ghafla wakaanza kuwashambulia askari kwa risasi.

Askari Polisi walijibu mapigo na kuanza kupambana na watu hao. "

Katika mapambano hayo askari Polisi walifanikiwa kuwajeruhi kwa risasi watu wanne katika kundi hilo la wahalifu  hao.

Aidha katika mapambano hayo zilipatikana silaha mbili aina ya Smg na magazine mbili pamoja na risasi 17 zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao.

Watu hao wanne ambao wanasadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaendesha vitendo vya mauaji katika wilaya za Mkoa wa Pwani.

Majeruhi hao walifariki dunia wakiwa njiani kupelekwa hospitali kutokana na kuvuja damu nyingi zilizotokana na majeraha ya risasi waliyopata, milli ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Jeshi la Polisi linaendelea kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi zitakazosaidia kuwakamata watu wanaojihusisha na vitendo hivi vya kihalifu kwenye wilaya za Mkoa wa Pwani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.