WATU wenye silaha wasiojulikana wametekeleza shambulizi katika soko nchini Sudan na kuua watu saba na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Habari nchini humo zinaarifu kuwa,
tukio hilo lilitokea Jumapili ya jana huko katika jimbo la Kordofan
magharibi ambapo watu wenye silaha wasiojulikana wakitumia magari ya
kiraia walishuka kutoka katika magari hayo na kuanza kuwafyatulia risasi
watu waliokuwa sokoni. Hadi sasa hakuna kundi lililotangaza kuhusika na
hujuma hiyo.
Inafaa kuashiria kuwa, waasi wa majimbo ya Kordofan kusini na Blue Nile wanapambana na jeshi la serikali ya Khartoum tangu mwaka 2011. Mapigano huko Darfur, yalianza mwaka 2003 baada ya makabila ya eneo hilo kuituhumu serikali ya Rais Omar al-Bashir wa Sudan kwa kufanya ubaguzi dhidi yao. Ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa, katika mapigano yaliyojiri maeneo ya machafuko nchini humo, karibu watu laki tatu waliuawa Darfur na zaidi ya wengine milioni mbili na laki tano kuwa wakimbizi.
Kwa kawaida raia wa kawaida ndio huwa wahanga wa mashambulizi ya
waasi na askari wa serikali. Mwanzoni mwa mwezi Machi uliomalizika
shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International lilitoa
wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu mashambulizi ya silaha za kemikali
yaliyofanywa na serikali ya Sudan dhidi ya raia wa kawaida katika eneo
la Darful, magharibi mwa nchi hiyo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.