ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 5, 2017

WATOTO 336 WAMEAGA DUNIA NIGERIA KUTOKA NA "MENINGITIS"


MAMIA ya watoto wamepoteza maisha kutokana na homa ya uti wa mgongo nchini Nigeria, huku duru za kiafya zikiarifu kuwa yumkini ugonjwa huo ukasambaa na kuenea katika nchi jirani ya Niger.
Taarifa iliyotolewa jana Jumanne na maafisa wa afya Nigeria na kimataifa mjini Abuja imesema kuwa, watoto 336 wenye umri kati ya miaka 5 na 14 wamefariki dunia kutoka na ugonjwa huo unaojulikana kwa Kiingereza kama 'meningitis' katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Imeogeza kuwa, kesi 2,997 za ugonjwa huo zimeripotiwa katika majimbo ya Zamfara, Katsina, Kebbi, Niger na Sokoto katika maeneo ya kaskazini magharibi na kaskazini ya kati nchini humo.


Ramani ya Nigeria
Kituo cha Kudhibiti Magonjwa nchini Nigeria (NCDC) kimebainisha kuwa, homa ya uti wa mgongo iliua watu 33 mwaka uliopita wa 2016, huku wengine zaidi ya elfu 2 wakiaga dunia kutokana na ugonjwa huo mwaka 2009. Aidha watu 1,100 walipoteza maisha kutoka na mlipuko wa ugonjwa huo katika nchi za Nigeria na Niger mwaka 2015, ambapo kesi elfu 10 ziliripotiwa.
 
Meningitis au homa ya uti wa mgongo ni ugonjwa unaosababishwa na virusi au bakteria, ambapo tishu zinazozunguka ubongo na uti wa mgongo wa muathiriwa huungua na kudhoofika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.