ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 17, 2017

NAIBU WA ZUMA AMTAKA ASIKILIZE MATAKWA YA WAANDAMANAJI.


Naibu Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema viongozi wanapaswa kuwasikiliza waandamanaji nchini humo ambao wanamtaka Rais Jacob Zuma ajiuzulu au aondolewe madarakani baada ya mabadiliko yake ya baraza la mawaziri kupelekea nchi hiyo kushushwa kiwango cha kiuchumi.
Zuma anatazamiwa kuachia ngazi kama mwenyekiti wa chama tawala cha ANC mwezi Desemba lakini muhula wake wa pili wa urais utamalizika baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2019. Ramaphosa na mke wa wamani wa Zuma, Nkosozana Dlamini-Zuma ni kati ya walio mstari wa mbele kuchukua nafasi ya Zuma.
Inaaminika kuwa Zuma anamuunga mkono mke wake wa zamani, huku Ramaphosa, mfanyabiashara tajiri na mkuu wa zamani wa vyama vya kutetea haki za wafanyakazi, akiwa na uungaji mkono miongoni wa waitifaki wa ANC katika sekta ya leba.
Maandamano ya wananchi dhidi ya Rais Zuma wa Afrika Kusini
 
Matamshi ya Ramaphosa ni tafauti na ya Zuma ambaye anawatuhumu waaandamanaji kuwa wana malengo ya ubaguzi wa rangi katika kumtaka aondoke madarakani. 
 
Chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance na vyama vingindgine vidogo vinaamini kuwa vinaweza kupata uungaji mkono katika kumuondoa Zuma baada ya hatua yake tata ya kumfuta kazi Waziri wa Fedha Pravin Gordhan aliyekuwa akiheshimika kitaifa na kimataifa.
 
Wakati huo huo Zuma amesema hatajiuzulu huku akisema anapingwa kwa sababu anazungumza haki. Akizungumza kanisani huko KwaZulu-Natal wakati wa pasaka amesema wakati umefika kwa Waafrika wazalendo kufurahia matunda ya uchumi.
Mahakama ya Katiba Afrika kusini inasikiliza kesi kuhusu iwapo kura ya kutokuwa na imani na Zuma bungeni ifanyike wazi au kwa siri. Wapinzani wanaamini kuwa iwapo muswada huo utafanyika kwa njia ya kura ya siri utafanikiwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.