ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 5, 2017

CHADEMA, CUF VYATINGA MAHAKAMANI KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI EALA



Twaha Taslim aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki pia Mwanasheria wa CUF 

VUGUVUGU la Uchaguzi wa wabunge wa Afrika Mashariki wazidi kulitikisa bunge. tayati Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na Chama Cha Wananchi CUF vimepanga kutinga mahakamani kupinga matokeo hayo.


Jana Mweyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe alitoa kauli ya kupinga matokea hayo mahakamani kutokana na kudai kuwa uchaguzi huo ulikwenda kinyume na taratibu za uchaguzi.


Leo akizungumza na Muungwana Blog kaimu Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Ahmed Katani, amesema kuwa uchaguzi huo umeendeshwa kinyume cha taratibu na kanuni za uchaguzi huo.


Amesema kuwa jana majira ya saa 8 na dakika 37 kabla ya uchaguzi huo alipokea  barua kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi Dk, Thomas Kashililah. Kwa mujibu wa barua hiyo ya Msimamiza wa uchaguzi ambayo alikiri kuwa kwa wagombea wa CUF kuna matatizo na kwamba hatuweza kushiriki kuchaguzi.


Katani amesema aliandika barua kwenda kwa msimamizi wa uchaguzi huo Dk Kashililah aliyopinga majina ya walidaiwa kuwa wagombea wa CUF ambao hawakufuta tararibu ndani ya chama hicho.


Amesema kuwa Mohammedi hatibu Mnyea ambaye sio mwanachama chama hicho na alishafukuzwa kwenye chama, lakini pia mgombe mwengine ni Thomas Malima ambaye alijitoa jana ambapo kanuni zinasema kuwa mtu anatakiwa kujitoa siku tano kabla ya uchaguzi lakini pia  mgombea huyo sio mwanachama wa chama hicho.


Pengamizi jengine ni juu ya Sonia Magogo ambaye ni Mwanachama ambaye hakufuata taratibu za uteuzi ndani ya CUF.


Katani amesema kuwa utaratibu ndani ya chama ni kikao cha Baraza kuu la Chama ndio lenye mamlaka ya uteuzi huo.


Amesema kuwa chama hicho kitaaenda Mahakamani siku ya juma tatu kupinga matokeo ya uchaguzi huo  kabla ya kuapishwa kwa wabunge hao

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.