ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, March 9, 2017

DAKIKA 90 ZATOSHA KWA BARCELONA KUIBADILI NYEKUNDU KUWA BLUE.


Barcelona wamebirua matokeo ya kutinga nusu fainali kwa kuizaba Paris Saint Germain kwa mabao 6-1 katika mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Ulaya.

Sergi Roberto alifunga bao la 6 kwa mkwaju wa mwisho wa mchezo, na hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa 6-5 kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Nou Camp.Barcelona walifunga magoli matatu katika dakika saba za mwisho. Walikuwa wakiongoza kwa 3-1. 

Wiki tatu zilizopita PSG iliifunga Barcelona magoli 4-0 mjini Paris.

Hatua ya kurejesha magoli yote hayo ni kubwa kuwahi kushuhudiwa katika historia ya UEFA, na sasa Barcelona wana kila nafasi ya kunyanyua kombe la Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu.

Katika mchezo mwingine, Pierre Emerick Aubameyang alipachika 'hat trick' na kuipeleka Borussia Dortmund katika robo fainali dhidi ya Benfica

Borussia Dortmund wameshinda kwa jumla ya magoli 4-1 katika mechi mbili walizocheza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.