ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 7, 2016

MAMA AFANYA UNYAMA KWA MWANAYE.

 TUNAOMBA RADHI KWA PICHA ZINAZOFUATA KWANI ZINATISHA NA KUSIKITISHA ILA ZIMEWEKWA HAPA KWAAJILI YA KUONESHA UKATILI ULIOFANYIKA. @gsengo

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 7.12.2016


·         MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMFANYIA UKATILI MTOTO MDOGO WA MWAKA MMOJA NA MIEZI MIWILI WILAYANI SENGEREMA.

KWAMBA TAREHE 6.12.2016 MAJIRA YA SAA 14:00 KATIKA KIJIJI CHA KILABELA KATA YA NYATUKULA WILAYA SENGEREMA MKOA WA MWANZA, MWANAMKE MMOJA ALIYEJULINA KWA JINA LA RHODA JUMA MIAKA 30, MUHA, MKULIMA NA MKAZI WA KIJIJI CHA KILABELA, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMFANYIA UKATILI WA KUMFUNGIA NDANI YA NYUMBA KWA MUDA WA MIEZI MINNE NA KUMSHAMBULIA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE MTOTO MDOGO WA KIKE MWENYE UMRI WA MWAKA MMOJA NA NUSU AITWAYE JULIANA KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.

INADAIWA KUWA MWANAMKE TAJWA HAPO JUU ALIKUWA AKIISHI NA MTOTO HUYO HAPO NYUMBANI KWAKE BAADA YA KULETEWA NA RAFIKI YAKE ALIYEJULIKANA KWA JINA MOJA LA RAHEL (RECHO) AMBAYE INADAIWA NDIO MAMA MZAZI WA MTOTO HUYO, AIDHA INASEMEKANA REHEL (RECHO) ALIMUACHA MTOTO HAPO KWA RAFIKI YAKE MWEZI  JULAI 2016, NA KWENDA KUSIKO JULIKANA KATIKA SHUGHULI ZAKE ZA UHUDUMU WA BAA.

AIDHA INADAIWA KUWA KWA KIPINDI CHOTE CHA MIEZI MINNE MTOTO ALIKUWA AKIFUNGIWA NDANI NA KUSHAMBULIWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA RHODA JUMA AMBAYE NI MAMA ALIYEACHIWA MTOTO, HALI ILIYOPELEKEA MTOTO KUWA NA MAKOVU MENGI MWILINI NA KUDHOOFIKA KIAFYA, WATU MAJIRANI WALIMUONA MTOTO HUYO WAKATI MAMA MWENYE KAYA ALIPOKWENDA KWENYE SHUGHULI ZAKE NA KUACHA MLANGO WAZI NDIPO WALITOA TAARIFA POLISI NA KUSAIDIA MTUHUMIWA KUKAMATWA.

MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA TAYARI AMEFIKISHWA MAHAKAMANI LEO TAREHE 7.12.2016, ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAKE, MTOTO AMELAZWA HOSPITALI YA WILAYA YA SENGEREMA AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU, HALI YAKE INAENDELEA VIZURI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA KUTENDA UKATILI WA AINA YEYOTE ILE KWA WATOTO AU WATU WAZIMA KWANI NI KOSA LA JINAI, ENDAPO IKIBAINIKA MTU ANATENDA UKATILI ATAKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA, HIVYO ANAWASIHI WANANCHI WATOE USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI ILI TUWEZE KUDHIBITI UKATILI KATIKA MKOA WETU WA MWANZA.

IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.