ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 9, 2016

SIMBA YALOWA TENA.


Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa katika dimba la Sokine kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Simba umemalizika jioni ya leo kwa timu wenyeji kuibuka na ushindi wa bao 2-1.

Licha ya kufungwa Simba ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kunako dakika ya 43, mfungaji akiwa Jamal Mnyate, aliyefunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya Shiza Kichuya  

HALF TIME:

Mwamuzi anapuliza kipenga kukamilisha kipindi cha kwanza cha mchezo huu. Timu zote zinaelekea vyumbani kupumzika.

Safari ya ushindi kwa wenyeji Prisons ilianza rasmi kunako dakika ya  48, baada ya timu hiyo kupata bao la kusawazisha mfungaji akiwa ni Victor Hangaya, aliyefunga baada ya kuunganisha mpira wa krosi ya Kimenya.

Dakika ya 63: Prisons wanapata bao la pili, mfungaji ni yuleyule Hangaya, anafunga kwa kichwa na kwa staili ileile. Ilipigwa mpira wa pembeni mabeki wa Simba wakafanya uzembe, akaruka juu na kufunga.
Hadi dakika 90 zinamalizika mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho, Tanzania Prisons wanaibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba.

KIKOSI CHA SIMBA 
1.Agban Vicent, 2 . Hamad Juma. 3.Mohamed Hussen, 4.Novaty Lufunga, 5 . method Mwanjali, 6 . Jonas Mkude, 7.Shiza Kichuya, 8.Mzamiru Yasssin, 9.Laudit Mavugo, 10.Mwinyi Kazimoto, 11.Jamal Mnyate. 

Sub:
Peter Manyika, Emmanuel Simwanza, Said Hamis, Mohamed Ibrahim, Ndusha Mussa, Haji Ugando

KIKOSI CHA TANZANIA PRISONS 
1. Andrew Ntala, 2. Salum Kimenya 3. Leonsi Mutalemwa, 4 . Jumanne Elfadhili 5. James Mwasote 6 . Kazungu Mashauri, 7. Lambarti Sabiyanka, 8. Mohamed Sammata 9. Victor Hangaya, 10. Salum Bosco 11.Benjamin Asukile

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.