ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 6, 2016

MWIGULU ACHARUKA TUKIO LA KUPIGWA MWANAFUNZI MBEYA. MWALIMU WA SHULE HUSIKA AZUNGUMZA NA JEMBE FM

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba 


Wakati Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akiagiza hatua kali zichukuliwe dhidi ya walimu wa shule ya Mbeya Day wanaodaiwa kumshushia kipigo mwanafunzi, MKuu wa Shule na baadhi ya walimu wamechukuliwa na polisi kwa mahojiano asubuhi leo.

Hatua hiyo imekuja  baada ya video kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha mwanafunzi  huyo wa kidato cha tatu, Sebastian Chinguka akipigwa kikatili na walimu.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 28 baada ya mwanafunzi huyo kutofanya zoezi la somo la Kiingereza.  

Zinaeleza kuwa walimu waliofanya kitendo hicho walikuwa kwenye mafunzo kwa vitendo. 

Sasa baada ya sauti ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba kusikila akilaani kile kilichotokea na kuapa kulifuatilia suala hilo Jembe Fm kupitia kipindi cha KAZI NA NGOMA Kinachoruka hewani kila siku saa 5 kamili hadi saa 7 mchana ilimtafuta Mwalimu Mkuu wa Shule kulikotokea sakata hilo.... BOFYA PLAY KUSIKIA KILICHOJIRI. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.