ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 12, 2016

JEH WAFAHAMU NI MWANAMUZIKI GANI ASHA BARAKA ASIYE MTAMANI KUMUONA AKIJIUNGA AU KUREJEA TWANGA?

BOFYA PLAY KUSIKIA MAZUNGUMZO. Mkurugenzi wa Bendi ya African Stars Twanga Pepeta 'The Iron Lady' ambaye pia ni Mjumbe wa NEC, Mama Asha Baraka amefunguka masuala mengi yanayoendelea ndani ya bendi yake, upepo wa kuingia na kutoka kwa wanamuziki, mikakati ya msimu wa kujiimarisha kwa kuwa na safu ya wasanii mahiri ikiwa ni sambamba na kurudisha wanamuziki wake wote waliokuwa tegemeo na mengineyo.

'Iron lady' amefunguka hayo wakati akihojiwa na mtangazaji Albert G. Sengo wa kituo cha redio Jembe Fm cha jijini Mwanza, kupitia kipindi cha SATURDAY XPRESS knachoruka kila Jumamosi saa moja kamili asubuhi hadi saa nne asubuhi.

Asha Baraka amesema licha ya ukumbi wa Mango Garden uliopo jijini Dar es salaa kutumika kama kiwanja cha nyumbani hatua hiyo haijaiathiri hata kidogo bendi yake kukosa mapokezi mazuri mikoa mbalimbali hapa nchini na hata nje ya nchi kwani Twanga Pepeta imejitengenezea jukwaa la kuaminika kama bendi ya wadau na wapenzi wa muziki wa ukweli Afrika.

Mkurugenzi huyo amekiri kurejea kwa baadhi ya wanamuziki mahiri wa bendi yake akiwemo repa muimbaji Khalid Chokoraa na mwimbaji anaye subiriwa urejeo wake ni Charles Baba ambaye si muda mrefu atajiunga tena na kundi lake la zamani.

Vipi suala la HAMA HAMA kwa wanamuziki halioni kwamba linaharibu ladha asili ya Twanga Pepeta? Amesema hilo ni suala mtambuka katika ulimwengu wa sasa wa Biashara ya soko Huria ambapo halijahathiri tu tasnia ya muziki bali pia hata vyombo vya habari na mifano akaitaja......

Je kuzijua kwake fitna za mjini na kucheza rafu kwa baadhi ya bendi ndiyo sababu kwake kudumu ndani ya Tasnia ya muziki wa dansi?

SWALI LA KIZUSHI.
Je ni mwanamuziki gani anayetamani kumrudisha Twanga kwa hali na mali, kwa udi na uvumba?
Je unafahamu mwanamuziki gani asiyemtamani kuwona akirejea au kujiunga Twanga?Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.