ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, September 4, 2016

MAKONDA:- 'NAOGA MATUSI' KUHUSU BAKWATA

Dar  es  Salaam.  Zikiwa zinakaribia wiki tatu tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aahidi kujenga ofisi za kisasa za Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), amesema uamuzi wake umezidi kuibua vita kutoka kwa  watu wasiopenda maendeleo wakimshtumu kwa hatua hiyo.

Makonda aliahidi kujenga ofisi hizo za kisasa zenye ghorofa tatu zitakazogharimu Sh5 bilioni.

Hata hivyo, Makonda alisema hatishiki na hali hiyo, bali atazidi kumuomba Mungu ili afanikiwe katika jitihada zake za kuwaletea maendeleo wakazi wa Dar es Salaam.

 Alitoa kauli hiyo jana alipohudhuria kikao cha kutambulisha safu mpya ya viongozi wa Baraza la Vijana la Jumuiya ya Waislamu wa Dar es Salaam kilichofanyika Ukumbi wa Anatouglo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.