ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 27, 2016

CHILE WASABABISHA MESSI KUSTAAFU KUICHEZEA TIMU YAKE YA TAIFA?

Michuano ya Copa America imefikia tamati leo hii kwa mabingwa watetezi Chile kuendeleza ubabe wake dhidi ya Vigogo wa soka duniani Argentina.
Dakika 120 za mchezo huo zilishuhudia timu hizo zikienda suluhu ya bila kufungana. Mchezo huo ulitawaliwa na ubabe wa hapa na pale huku ikushuhudiwa timu zote mbili zikimaliza kipindi cha kwanza zikiwa na wachezaji 10 baada ya Marcelo Diaz wa Chile kulambwa kadi mbili za njano na kuwa nyekundu dakika ya 28 kabla ya Marcos Rojo wa Argentina kutolewa nje dakika ya 43 kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja. 
Katika upigaji wa penalti,Arturo Vidal wa Chile alianza kwa kukosa kabla ya Lionel Messi na Lucas Biglia kukosa kwa upande wa Argentina.
Hii inakuwa fainali ya pili ndani ya miaka miwili kwa timu hizi mbili kukutana katika hatua ya fainali amapo mara zote mbili Chile wamechukuwa kikombe hicho kwa mikwaju ya penalti. 
Fainali hizi zilichezwa mwaka jana nchini Chile na kurudiwa mwaka huu ikiwa ni maadhimisho ya miaka 100 tokea kuanza kwa michuano hii mwaka 1916.

MESSI


Wakati huo huo mshambulizi wa Argentina na klabu ya Barcelona Lionel Messi amestaafu kutoka soka ya kimataifa.
Mchezaji huyo bora zaidi duniani alitangaza hatua hiyo baada ya kukosa penalti iliyoiwezesha Chile kuilaza Argentina katika fainali ya mchuano wa Copa America.
"Kwangu mimi ,soka ya kimataifa ama hata kuichezea Argentina sitaweza tena.
''Nimefanya kila niwezalo.''
''Kwa kweli inaniumiza kuwa sijawahi kutwaa kombe lolote la kimataifa'' alisema mshambulizi huyo mwenye umri wa mia 29. CHANZO BBC

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.