ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 10, 2016

MAHAKAMA YA RUFANI YAIBUA MAZITO KESI YA KITILYA NA WENZAKE.


Mahakama ya rufani nchini imetengua uamuzi wa mahakama kuu juu ya kupinga kufutwa kwa shtaka la 8 la utakatishaji fedha katika kesi inayomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA Harry Kitilya na wenzake.

Hukumu hiyo iliyosomwa Mahakamani hapo na msajili wa mahakama hiyo Zahara Maluma ambaye alisema mbali ya kutenguliwa kwa uamuzi huo pia mahakama Kuu imeamulia kusikiliza rufani ya msingi ya DDP.

 Aidha mahakama ya rufani imebainisha kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Moses Mzuna alikosea kutoa maamuzi yaliyosema kufutwa kwa shtaka la 8 la utakatishaji fedha katika kesi inayo mkabili Kitilya na wenzake hakutamaliza ama kuathiri shauri hilo.

ZAIDI BOFYA VIDEO (HAPO JUU)


MAKONTENA 103 YA MAGOGO TOKA ZAMBIA NA DRC YAKAMATWA.


Jumla ya makontena 103 ya magogo yanayodaiwa kutoka Zambia na DRC yamezuiliwa katika bandari ya Dar es Salaam kwa madai ya kutokuwa na vibali maalumu.

WATANZANIA WAISHIO NJE WALALAMIKIA CHANGAMOTO MBALIMBALI IKIWEMO KUFANYISHWA NGONO.

Watanzania wanaofanya kazi nje ya nchi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kulazimishwa kufanya biashara ya ngono. 

WATUMISHI HEWA PASUA KICHWA MBEYA.

Watumishi hewa wameongezeka zaidi mkoani mbeya kutoka watumishi 68 hadi kufikia 170 na kuingizia hasara serikali zaidi ya Sh. Mil. 770.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.