ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 27, 2016

HUKUMU YA KESI YA DAUDI MWANGOSI.

Mahakamu Kuu Kanda ya Iringa imetaja siku ya tarehe 21 mwezi wa 7 mwaka huu kuwa ndio siku ya kutoa hukumu ya kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Channel TEN ,Daudi Mwangosi inayomkabili askari wa jeshi la polisi kikosi cha kuzuia ghasia FFU Pasificus Cleophace Simon.

Akitoa majumuisho ya kesi hiyo Jaji wa mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa Paul Kiwhelo amesema majumuisho yaliyotolewa leo ni moja ya matakwa sheria ili kuwa na mazingira bora ya kupata picha halisi ya shauri hilo la mauaji namba 25 la mwaka 2013.

Jaji kihwelo ameieleza mahakama kuwa mnamo tarehe 2 sept 2012 mtuhumiwa Pasicuos Simon alitenda kosa hilo la mauaji na endapo mtuhumiwa akithibitika kutenda kosa hilo kwa makusudi mtuhumiwa atakabiliwa na adhabu ya kifo.

Ameeleza kuwa jukumu la kuthibitisha kosa ni la upande wa mashtaka na linapaswa kufanyika pasipo kuacha chembe ya mashaka kwa kuzingatia ukubwa wa shauri lenyewe.

Wakitoa majumuisho ya mwisho mahakamani hapo baada ya kusikiliza majumuisho ya upande wa jamhuri na utetezi waungwana wa mahakama wamesema mtuhumiwa alitenda kosa la mauji bila ya kukusudia.

Shauri hilo la mauaji namba 25 la 2013 limepangwa kusikilizwa tena ktk hatua ya hukumu mnamo tarehe 21 mwezi wa saba mwaka huu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.