ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 1, 2016

KUHUSISHWA UBADHILIFU WA ZAIDI YA MILIONI 300 WAMSIMAMISHA KAZI MHANDISI WA JIJI LA MWANZA.


NA PETER FABIAN, MWANZA.

HALMASHAURI ya Jiji la Mwanza kupitia Kamati yake ya Uongozi na Fedha imemsimamisha kazi Mhandisi wa jiji hilo, Ezekiel Kunyalanyala, kwa tuhuma za kushindwa kusimamia vyema matumizi ya zaidi ya sh ml 300 fedha za miradi ya maendeleo zilizotolewa kwa matengenezo ya dharula.

Miradi hiyo ni ya kukarabatiwa jengo la machinjio ya jiji yaliyopo eneo la Nyakato Kata ya Mhandu, daraja la Mwananchi lililopo Kata ya Mahina, mitaro ya barabara za Kata za Mhandu, Mkuyuni na ukarabati wa Kituo cha kulelea watoto waisho katika mazingira magumu cha zamani kijulikanacho kama Kuleana katika Kata ya Nyamagana.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Meya wa jiji la Mwanza, James Bwire, alisema kwamba tayari agizo la Kunyalanyala kusimamishwa kazi limetekelezwa na ameisha kabidhiwa barua yake kutokana na kushindwa kusimamia matumizi ya fedha za miradi hiyo ambayo inaonekana kutekelezwa chini ya kiwango kulingana na thamani ya fedha zilizotolewa.

Meya huyo alieleza kuwa, Kuleana kilitakiwa kukarabatiwa kwa sh ml 19 kwa ajili ya kutumiwa na Idara ya Ustawi wa Jamii, lakini badala ya ukarabati ulioelekezwa, kimepakwa rangi na kuwekwa milango miwili tu na vitasa.

“Mhandisi huyo ndiye aliyependekeza na kuomba fedha hizo kwa ajili ya ukarabati wa kituo hicho, haiwezekani sh ml 19 ziishie kupaka rangi, chokaa na kutengeneza milango miwili tu, badala ya kukarabati sehemu zilizoelekezwa, huo ni wizi tusioweza kuuvumilia,” alichachamaa Bwire.

Alieleza kuwa, baada ya Kamati ya Fedha na Uongozi chini ya uenyekiti wake mbali na kutembelea kituo hicho pia walitembelea miradi ya Machinjio ya jiji yaliyopo Nyakato, Daraja la Mwananchi na ujenzi wa mitaro ya barabara ya Mhandu, walibaini ujenzi kuwa chini ya kiwango kulingana na thamani ya fedha zilizotolewa baada ya wataalamu wa  Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuja na kutembelea kabla ya kuidhinisha kwa matengenezo hayo.

“Halmashauri iliomba kujengewa machinjio mpya ya kisasa kupitia mradi wa mazingira wa LVMP II kwa thamani ya sh bl 1.7 kwa sharti la kukarabati jengo moja la stoo ya ngozi katika machinjio hayo ili litumike kama machinjio ya mda, jiji likakubali na kutoa sh ml 150 lakini ukarabati huo pia hauendi vizuri,” alidai.

Alieleza miradi mingine aliyodai na Kamati yake kutoridhishwa na usimamizi wake katika ujenzi wa daraja la Mwananchi (sh ml 110) na ujenzi wa mitaro ya Mhandu (ml 26) hivyo kumuagiza Mkurugenzi wa jiji, Adam Mgoyi amwandikie baraua ya kumsimaisha kazi Mhandisi Kunyalanyala na tayari ameisha kabidhiwa barua ya kusimishwa.

Meya Bwire ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mahina (CCM) wilayani Nyamagana, alimtaja mtumishi mwingine aliyesimaishwa kuwa ni Mwanasheria wa jiji hilo, Maksudi Bwabo kutokana na kulalamikiwa na  wadau (wafanyabiashara) wa jiji hilo wakati wa kukusanya mapato kuwatishia kuwapeleka mahakamani bila kuwapatia nafasi ya kujitetea.

“Mwanasheria huyo anadaiwa kutembea na kutoa Samansi mfukoni kutishia wadau hali ambayo tumeomba akae pembeni “naye kusimamishwa” ili kupisha uchunguzi wa malalamiko ya tuhuma hizo , pia kuwataka watumishi wa Halmashauri hiyo wabadilike na kuacha kufanya kazi kwa mazoea ukizingatia kasi ya serikali ya Dk John Magufuli haina mchezo katika kuwatumikia wananchi.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.