ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, March 13, 2016

KOZI YA MAFUNZO YA WALIMU WA MPIRA WA WAVU MKOANI PWANI KUFANYIKA MACHI 24

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA

CHAMA cha mchezo wa mpira wa wavu Mkoa wa Pwani (COREVA)  kimeandaa kozi ya mafunzo ya walimu wa mchezo huo yanayotarajiwa  kufanyika kuanzia mwezi  machi 24 hadi Aprili 1 mwaka huu wilayani Kibaha.

Akizungumza na Tanzania Daima Katibu mkuu wa Chama hicho Lonjini  Mzavas alisema kwamba wameandaa kozi hiyo kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa lengo la  kuweza kutoa mafunzo  ambayo yataweza kusaidia kuwapata walimu wa mchezo huo.

Aidha Katibu huyo alisema kwamba kozi hiyo itawahusisha baadhi ya  walimu wanaotoka katika  shule za msingi, sekondari pamoja na vyuo waliopo katika Mkoa wa Pwani ambao kupitia kozi hiyo itaweza kuwajengea uwezo katika ufundishaji  wa mpira huo.

 Alisema kwamba lengo lao kubwa la  kuandaa kozi hiyo ni kwa ajili ya kuwajengea uwezo walimu wa kuzitambua sheria  na taratibu mbali mbai zinazotumika katika mchezo  huo wa wavu ili na wao  waweze kuzitumia vema kwa kuweza  kuwafundisha wanafunzi  mashuleni kwao.

“Ndugu mwandishi mchezo huu wa mpira wa wavu katika Mkoa wetu wa Pwani ulikuwa upo nyuma sana lakini kwa sasa tumejipanga na safu yangu ya uongozi kwa ajili ya kuhakikisha tunajitaidi kutoa kozi mbali mbai amabzo zitaweza kuleta mabadiliko chanya katika tasnia ya mchezo huu wa wavu,” alisema Mzava.

Katibu huyo alibainisha kwamba katika kozi hiyo walimu hao watafundishwa mbinu mbai mbali kwa njia ya vitendo pamoja na nadharia ili kuhakikisha kwamba pindi watakapomaliza mafunzo hayo watakuwa ni mabalozi wazuri katika kuutangaza mchezo wa mpira wa wavu katika Mkoa wa Pwani na Taifa zima kwa ujumla.

Pia alisema kwamba walimu ambao wanahitaji kushiriki katika kozi hiyo wanatakiwa kuchangia gharama ya kiasi cha shilingi 50,000 kwa ajili ya masuala mbali mbali ya vifaa, chakula pamoja na mahitaji mengine ya msingi kwa ajili ya uendesheji wa kozi hiyo.

Katika hatua  nyingine alisema kwamba kozi hiyo itafundishwa na mkufunzi kutoka chama cha wavu Tanzania (TAVA) na kuongeza Wilaya zote za Mkoa wa Pwani zitashiriki katika mafunzo hayo, ikiwemo, Bagamoyo, Kibaha, Kisarawe,Mkuranga,Rufiji, pamoja na Mafia.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.