ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 25, 2016

LICHA YA CHANGAMOTO MWANZA IMEPANIA KUSHIKILIA REKODI YA JIJI SAFI AFRIKA.

 JIJI la Mwanza limetangaza mpango kabambe na kudumu wa kusafisha jiji, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha kampeni zake kuendelea kushika rekodi ya kuwa jiji safi Afrika Mashariki na hatimaye kuifikia rekodi ya jiji safi Afrika ambapo safari hii licha ya changamoto mbalimbali zilizoweza kujitokeza msimu wa mvua zinazoendelea malengo bado yameendelea kushikiliwa.

Mpango wa usafi shirikishi uko palepale kwa wananchi wa kila kaya, kila mtaa, maeneo ya biashara na huduma kushiriki kusafisha mazingira kwa pamoja kila jumamosi ya mwisho ya mwezi, ambapo tarehe ya mwezi huu February ni 27.

Lengo la mpango huo wa kufanya usafi ni kuhakikisha kuwa jiji la Mwanza, ambalo linakua kwa kasi kwa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara linakuwa safi muda wote hatimaye kuweka rekodi ya kuwa jiji safi Afrika.


Mkoa pamoja na wilaya zake umejipanga vyema kushiriki zoezi hilo ambalo ni sehemu ya muendelezo wa juhudi za kuboresha mazingira zilizo asisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanganyika, na kulitaka zoezi hilo kuwa endelevu. ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA
Mulongo anasema kabla ya mpango huo, jiji lilikuwa na mpango wake madhubuti wa kufanya usafi na kupitia mpango huo ofisi yake imegundua makosa na changamoto kadhaa ambazo zimekuwa zikifanywa na watendaji wasio waaminifu huku akiahidi kuwashughulikia.
“Tunataka kupanda mbegu kwa wananchi wetu ya kupenda usafi na kuchukia usafi kwa kutumia mikutano yetu ya hadhara katika ngazi za mitaa, vyombo vya uhabari na uhamasishaji wa vikundi vya ngoma na matangazo ya kawaida”, anasema Mgoyi.
Kauli ya RC Mkuu wa mkoa, Magesa Mulongo, inawataka wananchi wote kwenye maeneo kushiriki kikamilifu kwenye kazi ya usafi ili kulifanya jiji la Mwanza kuendelea kuwa safi. Katika kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu, anawataka wananchi wote kuweka mazingira yao katika hali ya usafi, ikiwa ni pamoja na kuchemsha maji ya kunywa.
“Tukubaliane na tukiri sote tuna jambo kubwa la kusimamia usafi kwenye maeneo yetu, maeneo ya misongamano ya watu, vivuko vyetu likiwemo eneo la soko la Mwaloni ambalo huingiza wafanyabiashara kutoka nchi za Kongo DRC na Rwanda,” anasema Mulongo.
Hadi kumalizika kwa mwezi Disemba 2015, jumla la watu 613 wameugua ugonjwa wa kipindupindu ambapo 263 ni kutoka Ukerewe, Ilemela kutoka 180 Sengerema 135, Nyamagana wagonjwa 29 na Magu sita kutoka Magu. Watu 19 walifariki dunia ambapo 13 ni kutoka Ukerewe, Sengerema watatu na mmoja kutoka Magu.
Anasema zoezi la kufanya usafi halina itikadi ni zoezi la uzalendo, kwa madai kuwa ugonjwa wa kipindupindu unampata kila mtu bila ya kuangalia dini, kabila au chama chake cha siasa. Anatoa onyo kali kwa watendaji na watumishi watakaotumia zoezi hili katika kuwasumbua wananchi huku wakiwatisha na kuwaomba rushwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.