ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 6, 2015

KAMA HAUJAWAHI KUITEMBELEA SHULE YAKO YA ZAMANI ULIYOSOMA, MFANO HUU UNAKUHUSU.

NYASECO Alumnae kundi la wadau waliosoma shule ya sekondari Nyamilama wilayani Kwimba mkoani Mwanza.

Wadau hao wanatembelea shule yao ya zamani na kukagua shughuli za uendeshaji na utoaji elimu ikiwa ni sambamba na kuzimaini changamoto zilizopo ambazo zinaendelea kuikabili shule hiyo BOFYA PLAY KUSIKILIZA

Bwana Mussa Ezekiel akitizama moja ya kengele aliyoiacha mwaka 1992.
Kushoto ni Mussa Ezekiel, katikati ni John Semakura na kulia ni Mirambo Mulela wakionyesha mazingira ya shule hiyo ambayo walisoma miaka ya 1992.
Edward Kobero ambaye ni mkuu wa shule ya Nyamilama Sekondary akionyesha uso wa furaha kwani haijawahi kutokea kutembelewa na wanafunzi waliosoma shuleni hapo na kurejesha fadhila, mwalimu huyo naye alisema kuwa amehamasika kwa ujio huo akikiri kuwa naye anawajibu kurejea shule aliyosoma zamani kuzibaini changamoto. 
Hapa walitembelea jiko ambalo waliliacha miaka hiyo ya 1993.
Hapo ni Mirambo Mulale akiwa kwenye chumba cha maabara ambacho pia ni changamoto.
Hawakuishia hapo walitembelea wanafunzi wa sasa shuleni hapo na kuwatia moyo.
NYASECO Alumnae,wanafunzi waliosoma katika shule ya Sekondari Nyamilama walipata fursa pia kutembelea mabweni ya shule hiyo na kujione hali duni iliyopo  wakiahidi kurejesha fadhila huku wakiwaasa wananchi na vijana wengine warudi kwenye shule walizosoma na kuzisaidia bila kusubiri mkono wa serikali.
Shimo la kisima cha zamani.
Kushoto ni John Semakura (L) Mussa Ezekiel (C) na Mirambo Mulela (R) wakiwa eneo la bwawa ambalo limetumika kwa miaka sasa kuhifadhi maji kwa matumizi ya shule hiyo.  
Mussa Ezekiel akionyesha lango la bweni la wasichana ambalo pia linachangamoto zake.
Vyoo vya shule vilivyotumika tangu enzi za Mwinyi.
Hapa kulikuwa na kisima.
Mbele ya ofisi za shule hiyo ya sekondari.
Nje ya mazingira ya shule.
Taswira na mazingira.
Ndani ya ofisi za mkuu wa shule ya sekondari Nyamilama.
Wakibadilishana mawazo na baadhi ya walimu wa shule ya Sekondari Nyamilama.
Wakiwa mbele ya bweni ambalo kwa sasa ni la wasichana.
Wadau hao wametoa wito kwa jamii kujenga tabia ya kuzisaidia shule walizosoma zamani ili kuhakikisha kuwa changamoto mbalimbali zinazojitokeza zinatatuliwa hivyo kukuza kiwango cha taaluma kinachotolewa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.