ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 28, 2015

MANGO GARDEN NYEUPE WIKI HII, BURUDANI NI MOJA TU …YAMOTO BAND NA MASHAUZI LEO USIKU

MANGO GARDEN NYEUPE WIKI HII, BURUDANI NI MOJA TU …YAMOTO BAND NA MASHAUZI LEO USIKU …Malaika hawapo Ijumaa, Twanga hawapo Jumamosi Kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi, ukumbi wa Mango Garden Kinondoni unapitisha wikiendi bila burudani yoyote na badala yake onyesho la Yamoto Band na Mashauzi Classic leo usiku ndio show pekee wiki hii katika ukumbi huo.

Kesho Ijumaa Malaika Band ambao hupiga hapo Mango kila Ijumaa, watakuwa Arusha mjini. Twanga Pepeta ambao hupiga Mango Garden kila Jumamosi, Jumamosi hii watakuwa Wenge Garden Ukonga.

Bendi ya FM Academia ambayo huibuka Mango Garden nakufukia viraka vya bendi zilizopata dharura ya kuhama ukumbi, Ijumaa hii itakuwa Polisi Kilwa Road wakati Jumamosi itakuwa Leaders Club katika tamasha la nyamachoma.

Yamoto Band watakwea jukwaa la Mango Garden Kinondoni leo usiku (Alhamisi, 28) kuonyeshana kazi na wenyeji wao Mashauzi Classic chini yake Isha Mashauzi.

 Ni onyeshoambalolimetekahisiazamashabikiwamuzikikutokananaukwelikuwavikundihivyoviwilihavijawahikukutanakatikakatikaonyesho la pamoja, ukiondoayalematamashayanayoshirikishawasaniiwengi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.