ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 30, 2013

MWILI WA NGWEA ULIANZA KUPATA UBARIDI KABLA YA KUFIKISHWA HOSPITALI, BUSHOKE NAYE ATHIBITISHA KUFARIKI KWA ALBERT MANGWEA

Moja kati ya marafiki wa karibu wa msanii albert Mangwea aliyekuwa karibu naye nyakati za mwisho za maisha yake aliyejitambulisha kwa jina la Goddy amezungumza na Amlifaya ya Clouds fm jioni ya leo ikiwa ni Live kutoka nchini Afrika ya kusini akihojiwa naye mtangazaji Milard Ayo na kusema kuwa mwili wa marehemu Mangwea kabla hajafikishwa hospitali ulikuwa tayari umepata ubaridi. 

Hivi ni nini sababu ya kifo cha Ngwea? ZAIDI SIKILIZA HAPA CHINI:

  BUSHOKE NAYE ATHIBITISHA KUFARIKI KWA ALBERT MANGWEA AWASHUKIA WATANZANIA WANAOZUSHA TAARIFA ZA VIPIMO VYA DAKTARI BILA KUFATA TAARIFA RASMI. 
Msanii wa muziki wa bongo flavour Bushoke ni mmoja kati ya watanzania walioko nchini Afrika ya kusini akifanya kazi ya sanaa kule, kwa upande wake amewalaumu watu wanaozusha taarifa za vipimo vya daktari kupitia mitandao wakimchafua marehemu kwa taarifa zisizofaa akiwataka kuwa waungwana na kusubiri taarifa rasmi.

Naye Brother Rick ni mmoja kati ya watanzania ambao wamebahatika leo hii kuonana na msanii aliyekuwa amezirai M2tha P na kuishuhudia hali yake, anasema kuwa kwa sasa inaendelea vizuri ametolewa toka katika chumba cha ICU na kuhamishiwa kitanda kingine chumba cha wagonjwa kawaida ZAIDI SIKILIZA HAPA CHINI:
Mwili wa marehemu Albert Mangwea unatarajiwa kuwasili nchini Juni mosi (1 juni 2013) saa 8 adhuhuri na itafanyika mipango kuwawezesha mashabiki, ndugu, jamaa na marafiki kuuaga siku ya jumapili ya tarehe 2 juni 2013 viwanja vya Leaders Club kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 6 mchana.

Majira ya saa 6 mchana siku hiyo ya jumapili msafara utaelekea mkoani Morogoro kwaajili ya mazishi yaliyopangwa kufanyika jumatatu ya tarehe 3 mwezi juni 2013 katika eneo la makaburi litakalopangwa.

Tutaendelea kukupa taarifa zaidi endelea kuwa nasi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.