ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 20, 2012

MFALME ANAYEKUJA ANAVYOTISHIA MAISHA YA MABONDIA WENGI AFRIKA!

Mtanzania Ramdhani Shauri atapanda ulingoni siku ya Idd pili kupambana na bondia Sande Kizito kutoka Uganda kugombea mkanda wa IBF katika bara la Africa katika uzito wa unyoya (Featherweight).
Shauri anayefanya mazoezi yake Ubungo, maeneo ya Mabibo na anafundishwa na kocha mzazi anayetamba kuwa na mabondia wenye nidhamu na vipaji vya hali ya juu.

Ramdhani Shauri ni bondia chipukizi mwenye umri wa miaka 19 na historia yake ya ngumi inafurahisha kila anayeisoma na kuisikia. Ana haiba nzuri inayovutia na anafananishwa na bondia Sugar Ray Leonard wa Marekani kutokana na haiba yake na upiganaji wake.

Sugar Ray Leonard alitamba katika miaka ya 70 na 80. Shauri ni Mfalme anayekuja na hivi sasa anatishia maisha ya mabondia wengi katika bara la Afrika.

Ramadhani Shauri ana nidhamu ya hali ya juu na maisha yake katika ngumi yanafurahisha kwa jinsi anavyoishi kwa nidhamu na kufanya mazoezi ya kujijenga katika ngumi. Katika maisha yake anajiepusha sana na matatizo ambayo vijana wengi wametumbukia kama vile uvutaji wa bangi, ngono zembe na mambo mengine yasiyo na malengo katika maisha.

Huyu ndiye kweli Mfalme anayekuja katika ngumi za kulipwa na nchi yetu imepata bahati kubwa sana kuwa na kipaji cha bondia kama huyu.
Mpambano wa Shauri umepewa jina la “The Rumble in the City of Heaven’s Peace” (Vurumai katika Jiji la Amani)
Watanzania, tumuezi mwenzetu Ramadhani Shauri anapopeperusha bendera ya Tanzania. Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

Imetumwa na; Onesmo Ngowi
Rais wa IBF bara la Afrika, Mashariki ya kati na Ghuba ya Uajemi
Rais wa kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC)

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.