ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 10, 2011

STARS YAONA MWEZI, YAIZIMA PALESTINA 1-0

NDOTO za kocha Jan Poulsen kupata ushindi wa kwanza katika mechi ya kimataifa imetimia baada ya jana timu yake, Taifa Stars kuilaza Palestina kwa bao 1-0 la Mrisho Ngassa, dakika ya 62 kutokana na kazi nzuri ya Mohammed Banka aliyetokea akitokea benchi kipindi cha pili.
MSHAMBULIAJI wa stars Mrisho Ngasa (kulia), akiwania mpira na beki wa Palestina Samer Mahmoud Amin.

Ngassa alifunga bao hilo kwa kumchambua kipa Abdallah Alsidawi kutokana na mpira wa Banka, ambaye alikuwa ameingia uwanjani dakika tatu kabla ya bao hilo.

Stars walikaribia kupata bao la pili dakika ya 88, lakini Bonny alikosa umakini na kushindwa kutumia pasi ya Mrope ambaye alikuwa amewapiga chenga mabeki lukuki wa Palestina.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.