ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, July 23, 2017

MAPACHA WENGINE WALIOUNGANA KIFUA NA TUMBO WAZALIWA MOROGORO.

WATOTO wengine wawili walioungana kuanzaia kifuani mpaka tumboni wamezaliwa kwa njia ya upasuaji katika hospitali ya Misheni ya Bwiga wilayani kilosa mkoani Morogoro.

Huku hali ya mama na watoto hao ikiendelea vyema na mapacha hao wakitimiza miezi 9 lakini wamewekwa katika chumba maalum kwaajili ya uangalizi zaidi.

Luka kimole ni baba mzazi wa mapacha hao anasema ni suala la kushangaza kupata watoto kama hao lakini kwakwe katu halichukulii kama mkosi bali neema ambayo imetoka kwa Mungu.

Kaimu Mganga mkuu wa hospitali ya Berega anasema kuwa hali hiyo kujitokeza hasa kwa miaka ya sasa ni kutokana na malezi ya ujauzito.

"Mara nyingi akina mama wanapokuwa wajawazito hushauriwa kutumia baadhi ya huduma za tiba, kwa mfano Ferav na Folic ambazo zinawasaidia kwakiasi kikubwa kuzuia watoto kuzaliwa katika hali kama hizi lakini katika hili hatuwezi kuongea zaidi ni uchunguzi zaidi utafanyika kuona ni kwanini hali kama hzi hujitokeza kwa wingi hasa miaka ya hivi karibuni.

" Kwa nje waweza kuona kama watoto wawili ni vigumu kujua jeh kwa ndani ni miili ya wawili tofauti au kuna kitu kimoja wawili hao wanashare hivyo inaweza kufanyika huduma ya kutengenisha au lah.......

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.