ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 30, 2017

UJASIRIAMALI MPYA WA DIAMOND KATIKA PICHA.

NA:- Abog
Nyota wa Bongo Flava Diamond Platnumz ameendelea kuushika mtaa na mara hii sio kuachia ngoma kama ambavyo amefanya wiki chache zilizopita alipoachia nyimbo mbili kwa mpigo (I miss you na Fire) lakini sasa amerudi kwenye bidhaa zenye brand yake kama alivyoanza na Nguo kabla ya kutambulisha Manukato yanayotambulika kama Chibu Perfume.

Ili kuhakikisha anamfikia kila shabiki wake nchini kote bila kujali kipato chake ameingia kwenye biashara ya vyakula, ambapo Juni 29, mwaka huu, ametambulisha Karanga zake ambazo zitapatikana nchini kote. Karanga hizo zimefungwa kwenye mfuko mdogo ambapo kila moja itakuwa inauzwa kwa shilingi mia tatu 300/=

Diamond Platnumz pamoja na Label yake ya WCB Wasafi wamepata mafanikio mwishoni mwa wiki iliyopita Juni 25, baada ya msanii Rayvany kutwaa tuzo ya BET katika kipengele cha Best International Viewers Choice Award.

 PICHA KUTOKA KWENYE UTAMBULISHO WA KARANGA ZA DIAMOND.

Huku wasanii wengi wakitumia muda wao mwingi kuuza tisheti, Diamond alianzisha manukato ya Chibu ambayo ni bidhaa ya kipekee.

Msanii huyo baadaye alifanya kile ambacho wengi hawakutarajia kwa kuzindua njugu karanga siku ambayo alimkaribisha Rayvanny nchini Tanzania.

Hivi ndivyo alivyoandika katika chapisho lake la akaunti yake ya facebook siku ya Alhamisi:
USISEME KARANGA SEMA DIAMOND KARANGA!!!!...Habari njema kwa Vijana wenzangu wote, sasa unaweza kujipatia Mtonyo wa ChapChap kupitia @diamondkaranga ambapo utaweza kununua kwa bei ya jumla ya shilingi elfu ishirini (20,000) kwa boksi moja lenye pakiti Mia moja (100) ndani ambazo ukiuza unapata faida ya elfu kumi fanya mawasiliano sasa na mawakala walio karibu yako.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.