ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, May 21, 2017

KWA MAGOLI 14 MSUVA NDIYE MFUNGAJI BORA WA LIGI KUU TANZANIA BARA.

Kiungo wa Yanga Saimon Msuva amefanikiwa tena kuwa mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania Bara baada ya kufikisha mabao 14 yaliyosaidia kwa kiasi kikubwa timu yake kutwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa mara ya tatu mfululizo.

Msuva ambaye ni miongoni mwa wachezaji waliocheza kwa kujituma zaidi msimu huu amefanikiwa kuwakimbia wenzake waliokuwa wakimfukuzia kwa karibu nafasi hiyo ambao ni Abdulrahman Musa wa Ruvu Shooting aliyebaki na mabao 13.

Wengine ni Shiza Kichuya wa Simba, Obrey Chirwa wa Yanga na Mbaraka Yusuph ambao wote wamebaki na mabao 12 kila mmoja.

Msuva ni sehemu ya safu kali zaidi ya ushambuliaji msimu huu ambayo ndiyo iliyofunika katika upachikaji mabao ikiwajumuisha Obrey Chirwa, Amis Tambwe na Donald Ngoma ambao pamoja na wengine wameifanya Yanga ipate ubingwa msimu huu kwa tofauti ya mabao licha ya kulingana point na wekundu wa Msimbazi Simba.

Yanga imemaliza ligi ikiwa na mabao 43 ambayo ni tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa wakati Simba ikiwa na mabao 33 kama tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, na hivyo kuipiku Simba kwa jumla ya mabao 10 ya kufunga.

Hii ni mara ya pili kwa kiungo huyo machachari wa pembeni kuibuka kinara wa ufungaji katika ligi hiyo, ambapo katika msimu wa 2014/15 aliibuka pia mfungaji bora.

Tofauti na misimu iliyopita, katika msimu huu, wachezaji wa kitanzania wamefanikiwa kufanya vizuri katika ufungaji, kwani katika wachezaji watano waliofanya vizuri zaidi, ni Obrey Chirwa pekee ndiye mchezaji wa kigeni aliyepenya katika orodha hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.