NA ANNASTAZIA MAGINGA,Mwanza
UONGOZI wa Timu
ya mbao fc usema wamejipanga kuhakikisha
timu yao inaibuka na ushindi katika mchezo wa nusu fainali wa kombe la FA dhidi
ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa hivi karibuni kwenye uwanja wa CCM kirumba
jijni hapa.
Mbao fc imeingia katika hatua hiyo baada ya kuitupa nje Kagera sugar kwa bao 2-1katika uwanja wa
Kaitaba mkoani Kagera huku Yanga ikitinga hatu hiyo kwa kuifunga Prisons bao
3-0 katika mchezo wa robo fainali uliochezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Ofisa habari wa Mbao fc Chrisant Malinzi ameiambia G
sengo blog kuwa uongozi wa timu hiyo umejipanga vizuri kuhakikisha kikosi cha
chake kinaibuka na ushindi katika mchezo huo ili kutinga katika hatua ya
fainali na kutwaa taji la kombe hilo.
“Hatutegemei
kupoteza mchezo huo kwani tumejipanga kufanya vizuri ili kutimiza malengo yetu
ya kucheza fainali kwa mara ya kwanza na kutwaa ubingwa wa kombe la FA” amesema
Malinzi
Ameeleza kuwa wamejipanga na kwamba hawana hofu yeyote na mchezo wa nusu fainali ya kombe
la FA dhidi ya Yanga utakaofanyika kwenye uwanja waon wa Nyumbani CCM kirumba ili kutimiza malengo .
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.