ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, April 2, 2017

BOKO HARAM WATEKA NYARA WASICHANA WENGINE NIGERIA.


KUNDI la kigaidi la Boko haram limeteka nyara makumi ya wanawake na wasichana nchini Nigeria. 
Wakazi wa maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria wanasema kuwa, wanachama wa kundi la Boko Haram wameteka nyara wasichana na wanawake wasiopungua 22 katika mashambulizi mawili tofauti. Shambulizi la kwanza limefanyika katika kijiji cha Bulka kilichoko karibu na mpaka wa nchi hiyo na Cameroon ambapo wasichana 18 wamechukuliwa mateka.

Ripoti zinasema wapiganaji wa Boko Haram pia wameshambulia kijiji cha Dumba karibu na Ziwa Chad ambako wameteka nyara wasichana wengine 4 na kuua mwanaume mmoja.

Badhi ya wasichana waliokombolewa kutoka kwa kundi la Boko Haram
Mwaka 2014 kundi hilo la Boko Haram liliteka nyara wanafunzi 276 wa kike waliokuwa wakisoma katika shule ya Chibok, Borno, Kaskazini mwa Nigeria. Baadhi yao wasichana hao walibahatika kutoroka na wengine kukombolewa lakini hatima ya kundi kubwa la wasichana hawa bado haijulikani hadi leo hii.

Zaidi ya watu elfu 20 wameuawa katika nchi za Nigeria, Cameroon, Niger na Chad tangu kundi hilo la kiwahabi na kigaidi lianzishe mashambulizi huko kaskazini mwa Nigeria mwaka 2009.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.